Wednesday, November 25, 2020

AZAM IKIBORESHA USHAMBULIAJI MBABANE SWALLOWS WANALOA KWAO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MAREGES NYAMAKA

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (Caf), Azam FC mwishoni mwa wiki iliyopita waliendeleza rekodi yao ya kupata matokeo bora katika ardhi ya nyumbani baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbanane Swallows ya Swaziland

Lakini licha ya ushindi huo mbele ya mashabiki lukuki waliojitokeza kwenye Uwanja wa Chamazi, Azam walionekana kuwa bora katika maeneo ya kiungo na  ukuta, huku wakiwa dhaifu katika eneo la  ushambuliaji.

Safu ya ushambuliaji ya Azam katika mchezo huo iliyoongozwa na straika  Mghana, Yahya Mohamed, ilionekana kupwaya kwa kiasi kikubwa licha ya viungo wake kutimiza majukumu yao ya kutengeneza nafasi za kutosha.

Udhaifu huo ulimfanya kocha wa Azam, Aristica Cioaba, kipindi cha pili dakika 15 za mwisho kufanya mabadiliko kwa kumtoa Yahya na nafasi yake kuchukuliwa na winga, Khamis Mcha.

Yahya ambaye alitua Azam wakati wa usajili wa dirisha dogo Desemba mwaka jana kwa lengo la kumwongezea nguvu fowadi mzawa, John Bocco, alipoteza nafasi nne za wazi katika mchezo huo dakika za 27, 31 na 31 ikiwemo krosi makini ya winga Ramadhani Singano ‘Messi’ dakika ya tano.

Mbali ya kufunga bao pekee la Azam kwenye mchezo huo, Messi naye alikuwa na tatizo la kupiga krosi fyongo, pia alizidiwa ubavu mara kadhaa na mabeki wa Mbabane ambao walimpokonya mipira kirahisi.

Naye winga, Joseph Mahundi, hakuwa kwenye ubora wake hiyo ilichagizwa na ugeni katika michezo ya kimataifa, hata aliyechukua nafasi yake kipindi cha pili Shabani Iddi hakuwa na madhara mbele ya mabeki wa Mbabane Swallows.

Hata  uwepo wa Shabani pia haukuwa na madhara kutokana na kutokuwa na  mbinu sahihi za kuwachomoka mabeki wa Mbabane Swallows, licha ya kupigiwa mipira kadhaa na Singano,  Bruce Kangwa na Salum Abubakar ‘Sure boy’.

Kutokuwa na  uzoefu wa mechi za kimataifa, hili nalo lilikuwa tatizo kubwa kwa kinda huyu katika kufanya uamuzi sahihi kama ilivyotokea dakika mbili kabla ya mpira kumalizika aliposhindwa kupachika bao akiwa yeye na kipa wa Mbabane Swallows, Sandile Ginindla.

Mcha kwa upande wake alionyesha uhai kiasi fulani katika safu ya ushambuliaji  na moja kati ya kazi zake nzuri ni pande alilompatia Singano ambaye alifunga bao pekee la Azam.

Kwa mantiki hiyo, kuna umuhimu benchi la ufundi la Azam kufanyia kazi mapungufu hayo ikiwemo kuhakikisha inaipika sawa sawa safu yao ya ushambuliaji kabla ya kucheza mechi ya marudiano itakayopigwa nchini Swaziland Machi 18.

Kitu kizuri ni kwamba, kuna matumaini ya kuwepo kwa mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo, John Bocco, katika mchezo wa marudio ambaye imeelezwa amepona majeraha.

Bocco ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa kikosi cha Azam, anaweza kutumia uzoefu wake katika michuano ya kimataifa kuisaidia kupata matokeo chanya katika mchezo wa marudiano.

Huku pia safu ya ulinzi inayoongozwa na Yakub Mohamed, kuendeleza uimara wake mara dufu kama mchezo wa awali Chamazi Complex. Pia safu ya kiungo iongeze umakini wa kutopoteza mipira kirahisi na kuwahitaji kukaba kwa wakati.

Vile vile Himid Mao ambaye ana wastani mzuri wa kukaba ikiwamo kupokonya mipira, kama ilivyo kwa Staphen Kingue endapo atakuwa amepona majeraha yake litakuwa chaguo lingine sahihi kucheza na nahodha huyo msaidizi.

Hiyo inatokana na upambanaji wa Kingue kutumia vema nguvu zake kweli kweli, itasaidia zaidi eneo hilo kutopitika kirahisi kuliko ilivyokuwa  kwa kina Sure Boy pamoja na Frank Domayo ambao ni wazuri sana wakiwa na mpira mguuni kuliko kukaba.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -