Saturday, November 28, 2020

Azam katika kibarua cha Ruvu Shooting

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAINAB IDDY,

WAKATI mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga ikichezwa leo, ligi hiyo itaendelea tena kesho katika viwanja vitano tofauti nchini.

Katika Uwanja wa Chamanzi Complex, wenyeji Azam watawakaribisha Ruvu Shooting kutoka mkoani Pwani, ambapo Wanalambalamba hao watakutana na wageni wao wakiwa wanatoka kupokea kipigo cha maboa 2-1 kutoka kwa Ndanda FC kwenye Uwanja  wa Nangwanda Sijaona, mkoani Mtwara.

Kwa kupoteza mchezo huo, Azam walishuka kwenye msimamo wa ligi kutoka nafasi ya pili hadi ya nne, ikiwa na pointi 10,  sawa na Yanga  waliopo juu yao kutokana na kubebwa na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa, huku Wanajangwani hao wakiwa wamecheza mechi tano tu, moja pungufu ya Wanalambalamba hao.

Kuelekea mechi hiyo, Azam wanahitaji ushindi ili waweze kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi ambayo Simba wanaongoza hadi sasa.

Mechi nyingine za kesho ni kati ya Mbeya City na Mwadui kwenye Uwanja wa Sokoine, mkoani Mbeya.

Ikumbukwe Mbeya City imetoka kupokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Ruvu, huku Mwadui wakitoka sare na Tanzania Prisons mechi zilizopita.

Kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea, wenyeji  Majimaji watawakaribisha wababe wa Yanga, Stand United, huku huko mkoani Kagera kwenye Uwanja wa Kaitaba, Tanzania Prisons wakiwa ni wageni wa Kagera Sugar.

Kwa upande wao, Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa African Lyon kwenye Uwanja wa Manungu Complex, mkoani Morogoro, wakati JKT Ruvu ikiwa ugenini katika Uwanja wa CCM Kirumba, mkoani Mwanza, kumenyana na Mbao FC.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -