Wednesday, January 20, 2021

AZAM KULIPA KISASI KWA KAGERA SUGAR

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA WINFRIDA MTOI

TIMU ya Azam FC inatarajia kushuka dimbani leo kwenye uwanja wao wa Azam Complex, Dar es Salaam, katika mchezo wa raundi ya tatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar.

Wiki iliyopita Azam walikutana na Simba katika uwanja huo na kutoka suluhu, lakini pia itakutana na Kagera Sugar ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa bao 1-0 kwenye uwanja huo.

Bao hilo pekee lilifungwa na Themi Felix, katika mchezo wa mwisho wa ligi hiyo na kuwaondoa Azam katika nafasi ya tatu waliyokuwa wanashikilia.

Hata hivyo, leo huenda Azam FC wakampa kazi maalumu mshambuliaji wake, Mbaraka Yusuf, kulipa kisasi kwa Kagera Sugar waliyemsajili kutoka kikosi hicho kinachonolewa na Mecky Mexime.

Yusuf ni miongoni mwa wachezaji aliyeisumbua safu ya ulinzi ya Azam siku hiyo, lakini hivi sasa ni mali ya  Wanalambalamba hao.

Akizungumza na BINGWA jana, kocha msaidizi wa timu hiyo, Idd Cheche, alisema lengo lao kubwa ni kushinda mchezo huo hivyo watapanga kikosi imara kitakachosaidia kupata matokeo chanya.

Alieleza kuwa msimu huu wamekuja kivingine na malengo yao ni ubingwa, hivyo michezo ya nyumbani kwao ni muhimu katika kuhakikisha wanapata pointi kwa kila mechi.

“Ni kweli msimu uliopita Kagera walitusumbua na kutufunga mechi ya mwisho, lakini msimu huu tumejipanga kupigania ubingwa hivyo tutahakikisha hatupotezi pointi hasa katika uwanja wa nyumbani,”  alisema Cheche

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -