Friday, December 4, 2020

AZAM KUMALIZIA HASIRA KWA YANGA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

CLARA ALPHONCE NA ZAINAB IDDY

BAADA ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na timu ya Mbabane Swallows ya Swaziland, Azam wamepanga kumalizia hasira kwa Yanga.

Azam waliondolewa kwenye michuano hiyo kwa jumla ya mabao 3-1, ambapo katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, wenyeji Azam walishinda bao 1-0, lakini walifungwa mabao 3-0 waliporudiana na wapinzani wao nchini Swaziland.

Hata hivyo, Azam wamesema baada ya kuaga kwenye michuano hiyo, wanajipanga kikamilifu ili waweze kuibuka na ushindi dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Aprili mosi mwaka huu, Uwanja wa Taifa.

Meneja wa timu hiyo, Philipo Alando, alisema wachezaji wao wameanza mazoezi baada ya kurejea nchini wakitokea Swaziland.

Alando alisema lengo lao ni kutaka kuendeleza rekodi yao waliyoanza nayo kwenye Kombe la Mapinduzi Zanzibar ambako walifanikiwa kuzifunga Simba na Yanga.

Alisema wamerejea nyumbani na nguvu zao wanaelekeza zaidi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho (FA) kwani wana uhakika asilimia 100 ya kutwaa kombe hilo.

“Tuna asilimia 100 ya kuchukua Kombe la FA na asilimia 99 ya ubingwa wa Ligi Kuu, nafasi zaidi tunawapa Simba na Yanga ambao wanashika nafasi za juu katika msimamo wa ligi,” alisema Alando.

Katika hatua nyingine, Meneja huyo alisema wanatarajia kuwakosa baadhi ya wachezaji wao dhidi ya Yanga ambao ni majeruhi.

Aliwataja wachezaji hao kuwa ni John Bocco ambaye atakaa nje ya uwanja kwa kipindi cha mwezi mmoja na Aggrey Morris atakuwa nje ya uwanja wiki mbili kutokana na kuwa majeruhi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -