Tuesday, October 20, 2020

Azam kuvunja benki kusaji beki

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA SALMA MPELI

AZAM wanatarajia kuvunja benki kwa kusajili beki kisiki katika dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ulioanza Novemba 15 hadi Desemba 15 mwaka huu.

Uongozi wa Azam unatarajiwa kufanya hivyo baada ya Pascal Wawa kumaliza mkataba wake na kurejea katika klabu yake ya zamani ya El- Merreikh ya Sudan.

Akizungumza na BINGWA jana, Ofisa Habari wa Azam, Jafar Iddy, alisema baada ya Wawa kuondoka wanatafuta beki wenye uwezo mkubwa kwa lengo la kuongeza nguvu katika safu ya ulinzi.

Iddi alisema kwa sasa tayari wamesajili wachezaji watatu wa kigeni ambao ni washambuliaji Agyei Atta, Yahaya Mohamed na Samwel Afful kutoka Ghana.

“Tunatafuta beki wa kati kuchukua nafasi ya Wawa, lakini tayari tumeongeza nyota watatu kwenye kikosi chetu baada ya kuachana na wachezaji wengine watatu tuliokuwa nao awali,” alisema.

Iddy alisema wachezaji wao wanatarajia kuingia kambini Desemba 2 mwaka huu, kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuwapa mapumziko ya wiki mbili.

Alisema  wachezaji hao wanatarajia kuanza mazoezi baada ya makocha wa timu hiyo kurejea nchini wakitokea Hispania ambako walikwenda kwa mapumziko mafupi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -