Saturday, October 31, 2020

AZAM WAANZA KUIWINDA PRISONS

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SALMA MPELI

BAADA ya mapumziko ya siku moja kikosi cha Azam FC kimeingia kambini jana na kuanza mawindo yake dhidi ya Tanzania Prisons, mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili utakaofanyika Alhamisi hii kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Timu hiyo ilitarajiwa kuanza mazoezi yake jana saa 1:00 jioni kwenye uwanja wao, kujiandaa na mchezo huo baada ya kurejea wakitokea Songea walipotoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Majimaji kwenye mchezo uliopita.

Akizungumza na BINGWA jana, Ofisa Habari wa Azam, Jafari Iddy, alisema  kikosi hicho kinafanya maandalizi ya nguvu ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo huo ujao baada ya kupoteza pointi mbili kwenye mchezo uliopita kutokana na sare waliyoipata.

Alisema baada ya matokeo hayo kocha ameendelea kuwapa moyo wachezaji wake ili wawe na ari ya kuweza kuibuka na ushindi kwenye mchezo ujao.

“Timu ilipewa mapumziko ya siku moja baada ya kutoka safari ya Songea na kwa ajili ya Sikukuu ya Krismasi, inaanza mazoezi leo saa 1:00 jioni kwa ajili ya kujiandaa na mechi ijayo dhidi ya Prisons na tuajipanga kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo ili kujiweka kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hiyo,” alisema Jafari.

Azam ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa na jumla ya pointi 27 sawa na Mtibwa Sugar waliopo nafasi ya tano huku timu hiyo zikitofautiana idadi ya mabao ya kushinda na kufungwa, lakini zote zikiwa zimecheza michezo sawa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -