Wednesday, November 25, 2020

AZAM WAMPA JEURI NIYONZIMA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MWANDISHI WETU

BAADA ya kucheza vizuri kwenye mechi dhidi ya Azam FC na kutoa pasi ya bao pekee kwenye mchezo huo, kiungo  mchezeshaji wa Yanga, Haruna Niyonzima, ameanza jeuri baada ya kusema anahitaji  Dola elfu 50  za Marekani, sawa na  Sh milioni 100 za Kitanzania ili aweze kusaini mkakaba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya Jangwani.

Niyonzima amesema hatasaini mkataba iwapo hatapewa kiasi hicho na Dola 7000 za Marekani sawa na Sh milioni 14 za Kitanzania, ikiwa ni mshahara wake kila mwezi.

“Nataka Dola elfu 50 fungu la usajili na Dola 7000 mshahara wangu ndio nitaweza kusaini mkataba mpya ndani ya Yanga,” alisema.

Niyonzima ambaye amekuwa pia ni nguzo muhimu ya mabao Yanga, amesema katika maisha yake ya soka ndani ya Yanga, ametumikia timu hiyo kwa mapenzi ya hali ya juu na kamwe hajawahi kuihujumu.

“Sijawahi kuihujumu Yanga na nina mapenzi nayo ya dhati kabisa, nawashangaa wanaokuwa wananitaja pindi timu inapofanya vibaya au hata kuvurunda kuwa nimehusika,” alisema.

“Kama ningekuwa naihujumu Yanga, hivi naweza kukubali hela za mafungu za usajili alafu nikaacha hela za keshi za Simba ambazo waliwahi kuniwekea ili nijunge nao? Hilo jambo sijawahi kulifanya kwa sababu nina mapenzi ya dhati na Yanga,” alisema.

Akizungumzia ushindi wa juzi dhidi ya Azam, Niyonzima alisema siri kubwa ya ushindi huo ni kuweka matatizo yao pembeni na kupigana kwa ajili ya timu hiyo ili iweze kutetea ubingwa wake msimu huu.

“Tuliweka tofauti zetu pembeni na matatizo pia kwani Yanga tunadai mishahara, lakini tuliingia kwenye mchezo huo kwa ajili ya kuhakikisha tunapata pointi tatu kwa kuweka matatizo yetu pembeni,” alisema.

Katika hatua nyingine, Niyonzima hakusita kumuonya kipa wao, Deogratius Munish ‘Dida’, kuacha tabia ya kutoka mara kwa mara langoni kwa sababu imekuwa ikiwagharimu.

“Dida amekuwa na tabia ya kutoka sana kwenye eneo lake, ile ni hatari sana na inaweza kutugharimu simu moja,” alisema.

Niyonzima anaungana na wachezaji wengine Yanga ambao mikataba yao ipo ukingoni na huenda wasionekane tena ndani ya klabu hiyo kama hawataongezewa mikataba yao.

Wachezaji wengine ambao huenda wasionekana tena msimu ujao ni Dolnad Ngoma, Amissi Tambwe, Haruna Niyonzima, Thaban Kamusoko, Vincent Bossou, Nadir Haroub ‘Canavaro’, Kelvin Yondan, Oscar Joshua Ali Mustaph Batherz, Haji Mwinyi, Deogratius Munishi ‘Dida’ na Malimi Busungu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -