Monday, August 10, 2020

Azam yaipiga bao Yanga

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA WINFRIDA MTOI

KIUNGO wa Kagera Sugar, Awesu Awesu, ametua katika kikosi cha Azam baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili jana, akiwa mchezaji huru.

Awesu ni kati ya wachezaji waliokuwa wakitajwa kutua Yanga kwa msimu ujao kutokana na kiwango alichokionesha msimu huu.

Mchezaji huyo amekuwa wa kwanza kufungua usajili mpya wa Azam katika dirisha kubwa la kuboresha kikosi hicho kilichoshindwa kufanya vizuri msimu uliomalizika wikiendi iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Azam jana, mchezaji huyo alisaini mkataba huo mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Abdulkarim Amin ‘Popat’.

“Azam FC tunayo furaha kubwa kuwataarifu kuwa tumekamilisha usajili wa aliyekuwa kiungo wa Kagera Sugar, Awesu Awesu, kwa mkataba wa miaka miwili,” ilisema taarifa hiyo.

Akizungumzia kutua kwake Azam, Awesu, alisema amefurahi kurudi nyumbani kwa sababu aliwahi  kukaa katika kituo cha klabu hiyo kwa miaka miwili kuanzia  2014-2015.

“Siwezi kuahidi kuwa nitafanya nini, ila nina furaha ya kurejea nyumbani, Azam ni timu kubwa itakayonisaidia kufikia malengo yangu,” alisema Awesu.

Nyota huyo amekuwa na kiwango kizuri kwa misimu miwili mfululizo akiwa na Singida United na msimu huu Kagera Sugar, aliyoifungia mabao saba.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -