Wednesday, October 28, 2020

AZAM YAJIONDOA CAF

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SAADA SALIM


AZAM FC itakuwa na wakati mgumu kuweza kusonga mbele kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, kutokana na kuelekeza nguvu zao zaidi Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiziombea Simba na Yanga kupoteza michezo yao.

Ratiba iliyotolewa na Shirikiso la Soka la Afrika (CAF) hivi karibuni, imeonyesha kwamba Azam itasubiri mshindi kati ya  Mbabane Swallon na Opara United, ili kucheza nayo katika michuano hiyo.

Akizungumza na BINGWA jijini jana, Ofisa habari wa timu hiyo, Jaffer Iddy, alisema kwa sasa wanazielekeza nguvu zao katika mechi za ligi kuu.

“Kwa sasa tunafikiria jinsi ya kupambana na kufanya vizuri katika mechi zetu za ligi, suala la maandalizi ya michuano ya kimataifa tutajua katikati ya Februari,” alisema Jaffer.

Jaffer alisema wamejipanga kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye ligi kwa kuwa bado hawajakata tamaa kwenye mbio za ubingwa.

“Kwasasa akili zetu tumezielekeza kwenye ligi kwa kuwa hatujakata tamaa katika mbio za ubingwa, pia mechi hizo zitakuwa sehemu ya maandalizi.”

“Ila kwa sasa akili zetu bado ziko kwenye ubingwa, kwani ukiangalia wajuu yetu (Simba na Yanga) wakipoteza mechi mbili kila mmoja, huku tukipambana kuhakikisha tunashinda mechi zetu zote tutakuwa kwenye nafasi nzuri.”

Ofisa habari huyo alisema kulingana na ushindani uliopo katika ligi, wanaamini itawapa mwanga mkubwa hivyo watatumia vyema mechi hizo za ligi kuhakikisha wanajipanga kwa ajili ya michuano ya CAF.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -