Friday, December 4, 2020

AZAM, YANGA HADITHI NI ILE ILE WASIMULIAJI TOFAUTI

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA MAREGES NYAMAKA,

TIMU za Azam na Yanga ambazo zimekuwa zikiwakilisha Taifa katika michuano ya kimataifa kwa miaka ya karibuni ikiwamo msimu huu, zimekuwa na mwenendo wa kutoridhisha hasa kuishia hatua za awali, kwanza au makundi.

Azam ambao walikuwa upande wa Kombe la Shirikisho, safari yao ilifikia tamati mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kujikuta ikibamizwa mabao 3-0 dhidi ya Mbabane Swallows na kufanya matokeo ya jumla kuwa 3-1.

Hatua hiyo inaifanya Azam kuwa na rekodi mbaya zaidi ya kushindwa kupata matokeo bora ugenini na kuwaweka kwenye kundi la washiriki na si washindani.

Miongoni mwa mitanange waliyopoteza kwa idadi nyingi ya mabao ni dhidi ya El Merreikh iliyowabamiza 3-0 (2015), kipigo kama hicho Wanalalamba hao wakakumbana nacho tena mbele ya Esparance kama ilivyowatokea juzi Jumapili kwa Mbabane.

Huku michezo pekee iliyoonyesha ukomavu nje ya mipaka ya Tanzania ilikuwa dhidi ya Al Nasri Juba kwa kuifunga mabao 5-0, hatua iliyofuta ilifanikiwa kwa mara nyingine kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Barrack Young na baadaye wakapata ushindi mnono katika ardhi ya Afrika Kusini, ikiionyesha kazi Bidivest Wits 3-0 misimu tofauti.

Lakini hata hivyo, Azam haikuonyesha jitihada za kusonga mbele angalau hatua ya makundi kitu ambacho imekuwa mlima mrefu kuupanda, hiyo imechagizwa na mabadiliko ya mara kwa mara katika benchi la ufundi.

Pia, kushindwa kutumia vema uwanja wao wa nyumbani kupata ushindi mnono kama timu nyingine walizokutanazo kuwa mfano mzuri ni ilivyokuwa msimu huu walivyoshindwa kutumia nafasi nyingi Chamazi Complex na kujikuta wanaondolewa ugenini.

Kocha aliyepo kwa sasa, Aristica Cioaba ambaye alichukua mikoba ya Zeben Hernandes, Desemba mwaka jana, ndio kwanza amefikisha miezi mitatu hivyo isingekuwa rahisi kwenda mbali zaidi katika michuano hiyo.

Pamoja na madai ya hujuma waliyofanyiwa Azam kama baadhi ya matukio yalivyoonyeshwa kupitia televisheni, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu, Saad Kawemba, kufanyiwa fujo na mashabiki wa timu pinzani na vyumba vya wachezaji kupuliziwa dawa za kupunguza nguvu, lakini pia Mbabane walikuwa na kikosi bora.

Kutokana na ubora wa wapinzani wao hao tangu mchezo wa awali, licha Cioaba kulijua vema soka la Kiafrika na kuzinoa timu kubwa kama Raja Casablanca na Al-Masry, ingekuwa miujiza pekee ya soka kumvusha hatua inayofuata kwani alikuwa na muda kiduchu wa kuandaa timu hususani michuano mikubwa kama hiyo.

Vipi kuhusu Yanga?

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, katika mchezo wa marudiano dhidi ya Zanaco mjini Lusaka, Zambia, Machi 18, waliendeleza kucheza soka lao la kiwango cha juu muda mwingi wa mchezo wakishambulia kama nyuki lakini kitendo cha kuruhusu bao la nyumbani ilikuwa majuto kwao.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Mzambia George Lwandamina, awali kilicheza soka la kiwango cha chini katika uwanja wake wa nyumbani na kufanya mchezo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Yanga ambao pia msimu uliopita wakiwa chini ya kocha Mholanzi Hans van der Pluijm, waliishia hatua ya kwanza Ligi ya Mabingwa baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Al Ahly ugenini kutokana na kutoka sare ya bao 1-1 Uwanja wa Taifa.

Wanajagwani hao baada ya hapo wakaangukia pua katika Kombe Shirikisho na kuendeleza udhaifu wao wa kutotumia vema uwanja wa nyumbani, kwani baada ya kufanikiwa kuwatoa Sangrada Esperanca ya Angola kwa jumla ya mabao 2-1 na kwenda hatua ya makundi ilishinda mchezo mmoja pekee.

 Katika kundi hilo la timu kama Mo Bejaia ya Medeama na TP Mazembe, Yanga ilitumia vyema Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mo Bejaia na sare moja dhidi ya Medeama.

Mitanange iliyofungwa ni 1-0 Mo Bejaia, kipigo kama hicho kikitoka kwa TP Mazembe, kabla ya kuambulia vichapo vya 3-1 kwa timu za Medeama (Julai 26) na TPMazembe, Agosti 23 Lubumbashi.

Kulingana na yaliyotokea kwa Yanga na Azam, ni wazi yeyote hatakosea kusema kuwa hadithi imekuwa ni ile ile lakini wasimuliaji wakiwa ni tofauti, kwa vijana wa Jangwani safari hii akiwa ni Lwandamina badala ya Pluijm wa msimu uliopita na kwa upande wa wakali wa Chamanzi, akiwa ni Cioaba badala ya Hernandes.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -