Friday, October 30, 2020

BAADA YA KUIPIGA ‘HAT-TRICK’…

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA WINFRIDA MTOI


 

BAADA ya kuifunga Yanga mabao matatu ‘hat-trick’ katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juzi, mshambuliaji wa Stand United, Alex Kitenge, amesema anatamani mno kukichezea kikosi hicho cha Jangwani.

Katika mchezo huo, Kitenge ndiye aliyekuwa nyota wa kipute hicho kwa ‘hat-trick’ yake hiyo ambayo ni ya kwanza msimu huu.

Hata hivyo, mabao hayo hayakuisaidia Stand United kuepuka kipigo kutoka kwa Yanga baada ya kufungwa mabao 4-3.

Baada ya mchezo huo, Kitenge raia wa Burundi alizungumza na BINGWA na kuweka wazi jinsi anavyotamani kuitumikia Yanga, akiamini ana namba ndani ya kikosi cha kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera.

Kitenge alisema iwapo Yanga watamfuata na kumalizana naye na hivyo kutua Jangwani dirisha dogo, ataifanyia makubwa katika suala zima la kucheka na nyavu kwani huwa habahatishi katika hilo.

Alisema anaamini kutokana na uwepo wa Ibrahim Ajib na Mrisho Ngassa na nyota wengine katika kikosi cha Yanga, akitua Jangwani mashabiki wa timu hiyo watakuwa wakishangilia mabao kila mara.

Alisema japo ana uwezo wa kuichezea hata Simba, lakini amebaini Yanga ni sehemu anayoweza kupata namba kwa urahisi.

“Simba na Yanga zote ni timu na kubwa kwa Tanzania, wakinihitaji sina tatizo, kinachotakiwa ni kufuata taratibu ila Yanga naweza kucheza kwa urahisi kwa sababu wana mastraika wachache,” alisema Kitenge.

Alifafanua kuwa katika kikosi cha Stand United ana mkataba wa mwaka mmoja na una makubaliano ya kuondoka endapo atapata timu nyingine.

“Stand nilijiunga kwa mwaka mmoja, nilipomaliza mashindano ya Cecafa (Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati), nilikuwa nachezea timu ya Lydia Ludic ya Burundi na tumeelewana nikipata timu nzuri naweza kuondoka,” alisema Kitenge.

Katika kikosi cha Yanga kuna mshambuliaji mmoja tu wa kati ambaye ni tegemeo, Herieter Makambo, huku Matheo Anthony akiwa bado anasuasua, wakati Amissi Tambwe naye ndio ameanza kuwa fiti baada ya kusumbuliwa na majeraha kwa muda mrefu.

Kwa upande wa viungo washambuliaji, Yanga wanaonekana kuwa vizuri kwani wana Ngassa, Ajib na Deus Kaseke, huku nyuma yao kukiwa na kiungo Pappy Tshishimbi, Rafael Daudi, Japhary Mohammed, Thaban Kamusoko, Pius Buswita, Maka Edward na wengineo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -