Wednesday, September 30, 2020

BAADA YA KUJIUZULU SIMBA… Senzo atua Yanga

Must Read

KISA KONA YA CARLINHOS… ...

NA ZAINAB IDDY BAO la Yanga lililofungwa na Lamine Moro juzi katika mchezo dhidi...

HUYU MUGALU ATAWALAZA WATU NA VIATU TU!

NA ONESMO KAPINGA HAKIKA sijapata utamu wa mshambuliaji mpya wa Simba, raia wa DR...

Wachezaji Gwambina wapewa muda

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa timu wa  Gwambina, Fulgence Novatus, amesema amewapa muda wachezaji wake ...

MICHAEL MAURUS NA ASHA KIGUNDULA

KUNA sehemu ya mashairi ya wimbo wa mkali wa Hip Hop nchini, Fareed Kubanda ‘Fid Q’, yanayosema ‘akikupiga ngumi ya jicho na wewe mpige ya sikio, akikuuliza unaonaje na wewe muulize anajisikiaje’.

Ndivyo ilivyotokea baina ya watani wa jadi katika soka la Tanzania, Simba na Yanga ndani ya siku mbili tu, yaani juzi na jana.

Baada ya juzi Simba kumtangaza Bernard Morrison wa Yanga kama mchezaji wao, akionekana akisaini mkataba ndani ya jezi za Wekundu wa Msimbazi hao, Wanajangwani jana walidai kujibu mapigo kwa kumtwaa Ofisa Mtendaji Mkuu wa watani wao hao, Senzo Mbatha.

Pamoja na Yanga kusisitiza kuwa na mkataba wa miaka miwili na Morrison, Simba waliendelea kujinasibu kimya kimya kuwa Mghana huyo ni mali yao.

Kitendo hicho kilisababisha sakata hilo kufika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ikielezwa kuwa uamuzi wake wa aidha kubaki Yanga au kutua Simba, utatolewa leo.

Lakini wakati wapenzi wa soka nchini wakiendelea kutega masikio yao TFF, jana jioni zilizuka taarika kuwa Yanga wamejibu mapigo ya Morrison kwa kumnasa Senzo anayetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Simba msimu huu kwa kutwaa mataji matatu.

Imedaiwa kuwa moja ya sababu iliyomfanya Senzo kukubali kirahisi kuondoka Simba ni kitendo cha klabu yake hiyo kumsajili Morrison ambaye binafsi hamkubali kutokana na matukio yake ya utovu wa nidhamu tangu akiwa Afrika Kusini.

Lakini pia, inadaiwa kuwa Senzo hakufurahishwa na kitendo cha Simba kuwa katika mkakati wa kumtema kocha wao, Sven Vandenbroeck ambaye anamkubali mno, hasa kutokana na msimamo wake katika suala zima la nidhamu kwa wachezaji.

Ni kutokana na hilo, Senzo aliamua kujiuzulu wadhifa wake Simba kuanzia jana na kuposti katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter, akiishukuru klabu yake hiyo kwa muda wote aliofanya nao kazi.

“Natoa shukrani zangu kwa uongozi wa Klabu ya Simba kwa kunipa nafasi ya kuiongoza klabu kubwa kama hii. Kwa huzuni nimeamua kujiuzulu mara moja. Ndani ya kipindi kifupi, tumefanikiwa kufanya mengi. Ahsanteni sana Wanasimba,” alisema Senzo.

Mara baada ya posti yake hiyo, Mwenyekiti wa Bosi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’, alituma ujumbe uliosomeka: “Ofa nono ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL) yamuondoa Senzo Mazingiza Simba SC. Senzo ni miongoni mwa waliomba nafasi ya C.E.O katika Ligi ya PSL na mabosi wa PSL wamevutiwa na uwezo wa Senzo.

“Senzo washukuru viongozi na mashabiki wa Simba kwa ushirikiano. Kila la heri boss, umeacha alama ndani ya Simba SC.”

Lakini baada ya kusambaa kwa picha ya Senzo akionekana akisaini mkataba mbele ya watu wa Yanga, Mo alirudi tena katika mtandao na kutuma ujumbe uliosomeka: “Tumetoka mbali na bado safari inaendelea…nawaomba Wanasimba wote mtulie.

“Simba SC ni kubwa kuliko mtu mmoja. Sisi viongozi tunawatumikia usiku na mchana bila kujali maslahi ya mtu binafsi bali Simba, Kazi inaendelea, tuko imara.”

Baadaye alituma mara mbili mfululizo ujumbe mwingine uliosomeka: “Chunga kile ambacho umehangaika kukipata…Kila jema lina maumivu.” 

Naye Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Haji Manara alituma ujumbe uliosomeka: “Kwa hiyo mzunguko wa dunia umesimama siyo? Simba ni klabu kubwa, matumaini yetu kesho (leo) Senzo utakuja kukabidhi na nyaraka zetu kama utaratibu unavyosema…kifuatacho.”

Baadaya ya muda kidogo, Simba ilitoa tamko lililosomeka: “Klabu ya Simba imepokea kwa mshtuko uamuzi wa kujiuzulu wa Senzo Mbatha Mazingiza, kwa niaba ya klabu, tunaandika kuwajulisha umma kuwa klabu haitahusika na jambo lolote linalohusiana na Simba ambalo Senzo atafanya kwa sasa.

“Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi ya klabu, tunawashukuru wote kwa utulivu huku tukisubiri kutangaza Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu katika siku kadhaa zinazokuja.”

Mmoja wa wadau wa soka nchini, akiwamo aliyewahi kuwa mchezaji wa timu ya Kariakoo Lindi na timu ya Taifa, Taifa Stars Jemedari Said, aliandika kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram: “Aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mbatha, ameingia makubaliano na Yanga.

“Senzo ambaye ameandika barua ya kuacha kazi Simba SC leo (jana) mchana, amekamilisha makubaliano na mabosi wa Yanga SC na tayari ameshasaini kandarasi. Kilichobaki ni zoezi la kutangazwa rasmi ambalo litafanyika muda wowote leo (jana).
“Inasemekana moja kati ya sababu zilizomuondoa Simba SC ni pamoja na usajili wa winga wa Ghana aliyekuwa Yanga na kusajiliwa Simba, Mghana Benard Morrison.”

Baada ya taarifa hizo, BINGWA lilimtafuta Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, wadhamini wa Ynaga, Mhandisi Hersi Said kufahamu kama kuna ukweli wowote juu ya hilo.

Mara baada ya kupigiwa simu, Mhandisi Hersi alipokea haraka sana na kuanza kucheka kama vile alifahamu analotaka kuulizwa, lakini alishindwa kujibu lolote zaidi ya kuuliza: “Kwani na mimi ninaonekana katika hiyo picha (iliyomwonyesha Senzo akisaini mkataba Yanga), alipojibiwa ndiyo, alicheka na kukata simu.”

Mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye hakutaka jina lake kuwekwa wazi, alisema: “Inawezekana ni kweli kwani ninachofahamu mimi, toka juzi kulikuwa na mkakati wa kujibu mapigo ya Simba kwa kitendo chao cha kumng’ang’ania Morrison.”

Alisisitiza: “Hata kama ni kweli Senzo ametua Yanga, lakini bado kuna kishindo kingine, nadhani kesho (leo) iwapo TFF watamtangaza Morrison kama mchezaji wa Simba, kutatokea kishindo kingine kizito.”  

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

KISA KONA YA CARLINHOS… ...

NA ZAINAB IDDY BAO la Yanga lililofungwa na Lamine Moro juzi katika mchezo dhidi...

HUYU MUGALU ATAWALAZA WATU NA VIATU TU!

NA ONESMO KAPINGA HAKIKA sijapata utamu wa mshambuliaji mpya wa Simba, raia wa DR Congo, Chris Mugalu,kutokana na jinsi...

Wachezaji Gwambina wapewa muda

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa timu wa  Gwambina, Fulgence Novatus, amesema amewapa muda wachezaji wake  ili aweze kutathimini kiwango cha...

Kisu amfunika vibaya Manula

NA ZAINAB IDDY KIPA  wa timu ya Azam, David Kisu, amemfunika Aishi Manula  wa Simba kutokana na kutoruhusu...

Zahera awapa Simba taji mapema

NA ZAINAB IDDY BAADA ya Gwambina kufungwa mabao 3-0 na Simba  katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -