Wednesday, October 21, 2020

BADO SIMBA INAMUHITAJI JOSEPH OMOG

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA OSCAR OSCAR

UNADHANI tatizo ni fedha ndani ya Wekundu wa Msimbazi, Simba? Hapana. Pesa si tatizo kubwa. Ugeni umechangia kwa kiasi kikubwa sana kwa klabu ya Simba kukosa ubingwa kwa misimu minne ya hivi karibuni. Katika misimu hiyo, Simba haijawahi kumaliza hata msimu mmoja ikiwa na kocha yule yule wa mzunguko wa kwanza.

Bado Joseph Omog ni kocha bora ambaye mashabiki, viongozi na wanachama wa Simba wanapaswa kuendelea kumuunga mkono hata kama atakosa ubingwa msimu huu. Simba inahitaji kuwa na kikosi kilichokaa pamoja kwa muda mrefu, inahitaji pia kuwa na benchi la ufundi lililotulia ndani ya klabu. Kuingia na kutoka mara kwa mara kwa makocha na wachezaji kunairudisha nyuma sana klabu hiyo.

Baada ya Simba kupoteza mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi na kupoteza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc, wapo watu wanaoanza kumnyooshea kidole Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog. Kumekuwa na ugeni mkubwa sana wa makocha na wachezaji kila msimu, lakini bado matokeo yameendelea kubakia pale pale.

Ukiitazama Simba iliyocheza Michuano ya Mapinduzi na ukiitazama Simba inayocheza Ligi Kuu Bara msimu huu, unabaini utofauti mkubwa wa kuimarika kiwango tofauti na misimu iliopita. Joseph Omog pamoja na kufanya kazi kwenye mazingira yenye presha ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu, bado ameonyesha ufundi wa hali ya juu na utulivu.

Simba wamepoteza mechi tatu za ligi kuu msimu huu, lakini si kwa sababu ya mapungufu ya kocha, ni ubora wa wapinzani wao na kushuka viwango kwa baadhi ya wachezaji wa kikosi hicho. Omog anaonekana kuibadilisha Simba kwa kiasi kikubwa licha ya ugeni alionao ndani ya Msimbazi.

Wanasimba wanapaswa kuelewa kuwa Joseph Omog ni kocha wa daraja la juu, kumuondoa itakuwa ni kurudia makosa ambayo yamefanyika kwa misimu kadhaa iliyopita hivi karibuni. Kila kocha anakuja na mfumo wake na wachezaji wake, kumuondoa Omog ni kuifanya Simba kila msimu iwe inaanza upya. Moja kati ya sababu zinazoifanya Yanga kufanya vizuri, ni kukaa pamoja kwa wachezaji kwa muda mrefu na makocha wao. Simba na Azam FC wamekuwa na changamoto zinazofanana, kitu kinachoifanya Yanga izidi kuchanja Mbuga.

Kocha mgeni na wachezaji wageni wakati mwingine haiwezi ikawa rahisi kufanikiwa katika soka. Bado Simba wako kwenye nafasi nzuri, bado wanayo nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu. Tatizo mashabiki wa Simba wanachotaka ni kuona ushindi tu, hakuna ligi ya mtindo huo duniani. Jukumu la mashabiki ni kuishangilia timu yao, mambo ya ufundi aachiwe Omog. Narudia tena, kumuondoa Kocha Omog kutaendelea kuirudisha nyuma zaidi klabu hiyo.

Hata asipopata ubingwa msimu huu, bado naamini  kwamba Omog ni kocha bora ambaye atairudisha Simba kwenye ubora wake. Ushindani umekuwa mkubwa sana hasa mzunguko wa pili ambapo kila timu unayokutana nayo kama haitafuti ubingwa, basi inakwepa janga la kushuka daraja. Mashabiki, wanachama na viongozi wa Simba ni nafasi yao kumuunga mkono Omog, ana uwezo wa kuwapeleka kwenye ulimwengu wa furaha ambao kwa muda wa miaka minne umepotea pale Simba.

Nafahamu juu ya mkataba wake wa mwaka mmoja na naiona hatari ya Simba kuachana na Omog kama hawatachukua ubingwa, lakini huu ni utaratibu mbaya sana kwani kocha atakayekuja atakuwa mpya ambaye naye atakuja kuanza upya na si rahisi kumpata kocha aje kufanya miujiza kwa kujenga kikosi na kutwaa ubingwa.

Yanga ilijengwa na Ernie Brandts na Fred Felix Minziro, Hans van der Pluijm na Charles Boniface Mkwassa waliikuta ikiwa vizuri tu, walipoondoka, akaja Marcio Maximo alikuuta ikiwa timu imara, Pluijm aliporudi tena akaongoeza ubora ambao tunauona sasa ambao unaongezewa makali na Goerge Lwandamina. Hivyo naamini Simba inahitaji kuendelea na Omog baada ya msimu kumalizika, bila kujali mwisho wa msimu timu imetwaa ubingwa ama la, anachokifanya sasa ni kuijenga upya Simba ambayo itakuwa tishio zaidi misimu ijayo na si msimu huu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -