Wednesday, October 21, 2020

PLUIJM ASHIKWA UCHAWI YANGA

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI wa Ufundi wa Yanga, Hans van der Pluijm, ametajwa kuchangia kudorora kwa timu hiyo kutokana na ushawishi wake ndani ya wachezaji mabingwa hao wa Tanzania Bara.

Habari kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa Pluijm ameonekana kama hajaridhika kuporwa nafasi yake ya Kocha Mkuu na Mzambia George Lwandamina, hivyo kufanya mikakati ya chini kwa chini ili mwenzake huyo aonekane si mali kitu.

Kati ya mbinu anazodaiwa kuzitumia Pluijm kumharibia Mzambia huyo, ni kuwa karibu zaidi na wachezaji na kuzungumza nao kwa muda mrefu kuwafanya waamini yeye bado ni lulu Jangwani.

Mtoa habari wetu wa kuaminika amelipasha BINGWA akidai kuwa kuna wachezaji ambao Pluijm amewateka ili kusambaza ‘sumu’ kwa wenzao kumwona Lwandamina si lolote zaidi ya Mholanzi huyo.

“Kati ya mbinu anazozitumia ni kujifanya mtetezi wa wachezaji katika masuala mbalimbali, ikiwamo posho na nafasi ya kucheza, wengine wakiwa ni wale ambao yeye hakuwa akiwapa nafasi,” alisema mtoa habari wetu huyo ambaye hakupenda jina lake kuwekwa hadharani.

Aliongeza: “Huwezi amini, hata posho anashinikiza awepo kwenye mgawo wakati hakupaswa kupewa, ukizingatia analipwa mshahara mkubwa zaidi ya mtu yeyote kwenye benchi la ufundi.”

BINGWA lilimtafuta Naibu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit, kuzungumzia suala hilo, lakini simu yake ilikuwa haipatikani kama ilivyokuwa kwa Pluijm.

Wakati hayo yakiendelea, Pluijm ametajwa kuwapo katika mpango wa kuachana na Yanga na kutua Azam kuchukua mikoba ya Wahispania waliotimuliwa wiki iliyopita.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -