Wednesday, November 25, 2020

BALLON D’OR BILA RONALDO NA MESSI ITANOGA KWELI?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MADRID, Hispania

HIVI ulishawahi kujiuliza hafla za utoaji tuzo kwa mchezaji bora zitanoga vipi bila kumwona Cristiano Ronaldo au Lionel Messi akipanda jukwaani na kuzawadiwa tuzo huku wageni waalikwa wakimsindikiza na makofi ya pongezi?

Ni taswira isiyoelezeka, kwa sababu ni watu waliotesa mno kwenye tuzo hizo kwa kipindi cha miaka 10.

Na mapema wiki hii staa wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, alinyakua tuzo ya mchezaji bora wa dunia ya Fifa akimpiku mpinzani wake Messi ambaye amekuwa akichuana naye vikali kwa kipindi cha miaka hiyo 10.

Ronaldo alipewa nafasi kubwa ya kunyakua tuzo hiyo dhidi ya Messi na straika wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann, kutokana na mafanikio yake ya mwaka 2016, ambapo alichukua mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Euro 2016 na Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia.

Kama ilivyo kawaida, chenye mwanzo hakikosi mwisho. Je, tunaanza kuziona dalili za kuwakosa Ronaldo na Messi kwenye hafla za utoaji wa tuzo za kila mwaka?

Tangu Mbrazil Ricardo Kaka anyakue tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2007, hakuna mchezaji mwingine aliyeweza kuichukua tofauti na muungano huu wa ‘Ronaldo-Messi’, hata mshambuliaji huyo wa zamani wa AC Milan alivyochukua tuzo hiyo, Ronaldo alimaliza katika nafasi ya pili huku Messi akimaliza wa tatu.

Utawala wao umekuwa na nguvu mno kiasi cha kujinyakulia tuzo nyingine nyingi binafsi dhidi ya mastaa wengine duniani.

Miaka 10 kabla ya Ronaldo kuchukua Ballon d’Or mwaka 2008, kulikuwa na wachezaji 10 tofauti ambao walipokezana tuzo hiyo wakiwamo Zinedine Zidane, Michael Owen, Luis Figo, Pavel Nedved na Fabio Cannavaro ambaye alikuwa ni beki pekee kunyakua tuzo hiyo kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Lakini tangu 2008, wachezaji wazuri ambao kila baada ya misimu miwili au mmoja walikuwa na uhakika wa kunyakua mataji makubwa kama vile Xavi, Andres Iniesta, Thomas Muller, Wesley Sneijder, Andrea Pirlo na Gianluigi Buffon walishindwa kuibuka na tuzo hiyo ya mchezaji bora wa dunia.

Jibu la fumbo hilo ni hili; Messi na Ronaldo wanacheza soka la hadhi ya juu mno kuliko wapinzani wao hao, wanafunga sana mabao, wanashinda mataji na wamejitengenezea historia kubwa katika nafasi wanazozichezea.

Matokeo yake ndio tunayoyaona hivi sasa, tuzo wameifanya ya kwao na ndio maana tumeona Ronaldo akinyakua tuzo ya Ballon d’Or mwaka jana na mwaka huu kabeba ya FIFA, ni kwa sababu ya makubwa aliyoyafanya kwenye nyakati hizi.

Kiufupi, wakongwe hao wa ‘gemu’ wamefanya makubwa sana na kuing’arisha vita ya ‘Messi- Ronaldo’, lakini dalili zinaanza kuonesha kwamba si muda mrefu tutawakosa watu hawa kwenye tuzo.

Mwezi ujao Ronaldo atatimiza umri wa miaka 32. Ifikapo Juni mwaka huu Messi atakuwa na miaka 30 na kilichobaki ni kukubaliana na changamoto itakayowakuta ndani ya miaka michache ijayo kutoka kwa mastaa wanaoibuka hivi sasa.

Mwanzo una mwisho na kinapomalizika kipindi fulani basi ni wazi kingine kinakuja. Wababe hao walipokuwa kwenye kiwango chao wakiwa na umri mdogo tu hakukuwa na yeyote mwenye uwezo wa kuwafikia. Hivi sasa, wana jukumu la kupambana na nyakati kwani kizazi cha sasa kinakuja kwa kasi mno.

Gareth Bale na Luis Suarez ni wachezaji wanaonusa nusa kwenye anga zao hivi sasa, lakini kwa bahati mbaya wamejikuta wakitakiwa kuwasaidia Ronaldo na Messi katika klabu wanazocheza pamoja za Real na Barca.

Lakini bado mastaa hao wanao uwezo wa kuwapa changamoto Ronaldo na Messi mwaka huu, wakifuatiwa na Griezmann ambaye amekuja na moto.

Griezmann anatarajiwa kuondoka Atletico majira yajayo ya kiangazi na ni wazi kwamba atachagua timu yenye hadhi ya juu huku Manchester United ikizungumziwa kumhitaji. Kwa umri wake wa miaka 25, jamaa anao uwezo wa kufanya vizuri zaidi; ni mfungaji mzuri, ambapo kwa historia ya Ballon d’Or ufungaji wa mabao ni faida tosha itakayokupa nafasi ya kuichukua tuzo hiyo.

Halafu kuna Neymar Jr, bwana mdogo aliyepitwa mwaka mmoja tu na Griezmann, naye anagonga hodi kwenye anga za Messi na Ronaldo. Mshambuliaji huyu wa Barcelona ni nembo ya kizazi kichanga cha Brazil kinachotarajiwa kufanya mengi mazuri miaka ijayo.

Baada ya Neymar kuna huyu hapa, Paul Pogba. Mchezaji ghali zaidi duniani kwa sasa ambaye anaanza kuonesha ubora wake ndani ya kikosi cha United baada ya kipindi cha miezi kadhaa ya presha tangu aliposajiliwa kwa dau la pauni milioni 89.3 kutoka Juventus.

Wengi wanaamini kwamba, Pogba anao uwezo wa kuja kuwa kiungo bora ndani ya miaka 10 ijayo. Iwapo ataifanikisha klabu yake kurudi kwa kasi ndani ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mfaransa huyo atajidhihirisha kuwa alistahili kuwa mchezaji ghali.

Kwa sasa, ukumbi unamilikiwa na Ronaldo na Messi na ni wazi watazidi kupambana ili kushinda zaidi kwa sababu wanajua kwamba ubabe wao hautodumu milele.

Na inabidi wajiandae tu na changamoto hiyo, kwa sababu wachezaji wenzao hawawezi kufurahishwa na ubabe wao zaidi ya miaka 10. Na wao wanaitamani Ballon d’Or, wataitaka na tuzo ya Fifa pia.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -