Saturday, October 31, 2020

Balotelli huyu wa Nice achana naye

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NICE, Ufaransa

KOCHA wa Nice, Lucien Favre, alimpumzisha Mario Balotelli katika mchezo dhidi ya Nantes siku 10 zilizopita, lakini mchezaji huyo wa Italia alitoka akiwa na tabasamu kubwa.

Kumtoa dakika ya 75 ndio ilikuwa njia pekee ya kuweza kumpima Balotelli, ambapo kipimo hicho kilionyesha kwamba ana furaha sana kuwapo Nice.

Pia kumekuwa na mabadiliko makubwa hata katika maisha yake ya kawaida, akionekana kuachana na maisha yake ya zamani ya utata.

Tukio pekee la utata ambalo amelifanya akiwa Ufaransa ni lile la Agosti mwaka huu, baada ya kugongesha gari aina ya Bentley ya wakala wake, Mino Raiola wakati akiwa kwenye kumbi ya starehe.

Ukilinganisha na kipindi alipokuwa Inter Milan, Manchester City na Liverpool, Balotelli wa Ufaransa amebadilika na kuwa mwingine kabisa.

Pamoja na Nice kufungwa kwa mara ya kwanza mjini Caen, Balotelli amekuwa na mwanzo mzuri nchini Ufaransa. Akigongesha mwamba kwenye mechi hiyo waliyofungwa bao 1-0, akiwa amefunga mabao sita katika mechi sita za ligi alizocheza mpaka sasa.

Kiwango chake kizuri kimeisaidia timu yake kuwa kileleni mwa msimamo, wakiwa na pointi tatu juu ya Monaco na mabingwa watetezi PSG baada ya mechi 12.

Balotelli ameonekana kufanya vizuri kwenye kutengeneza nafasi za mabao na hata kusaidia timu kukaba na kuifanya Nice kuwa kwenye mbio za ubingwa wa Ligue 1 kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1959.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akifanya kazi kwa ajili ya timu yake, kitu ambacho ilikuwa nadra sana kukiona alipokuwa Ligi Kuu England.

Kuanzia siku ya kwanza alivyopokelewa kama mtu wao na kusifiwa kama Mungu, upendo alioonyeshwa na mashabiki wa klabu hiyo ndio sababu kubwa ya kucheza kwenye kiwango kizuri.

Nice ni klabu yenye mashabiki wenye shauku. Sasa Balotelli hana presha kama ilivyokuwa Liverpool, Milan au City. Pia ndio mchezaji mkubwa na staa wa timu, nyota ambaye wachezaji wengine wanamuangalia. Kiongozi kwa wengine, uwanjani na nje ya uwanja.

Kocha huyo wa Uswisi, Lucien, amemjenga nyota wake na kuwa fiti baada ya mchezaji huyo wa Italia kutokuwapo kwenye maandalizi ya msimu. Anamtia makali kwenye kupachika mabao na kushirikiana na mshambuliaji mwenzake Alassane Plea.

Balotelli kwa sasa ndio mfalme, jezi yake inauzwa sana kama chipsi kwenye migahawa maarufu na viongozi wa klabu hiyo wanasema wanauza jezi 10 za Balotelli kwa sasa. Msimu uliopita waliuza jezi 8,000 za Nice, lakini kuwasili kwa Balotelli, Nice wana matumaini ya kuuza jumla ya jezi 15,000 mwaka huu. Wakitarajia mashabiki 10,000 kuwa na jezi namba tisa ya Balotelli.

Kufuatia kuondoka PSG kwa mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic na kutua Manchester United, Ligue 1 ilihitaji shujaa mwingine na sasa wamempata mjini Riviera. Ambaye ni Balotelli.

Ilishangaza kuona kocha wa Italia, Giampero Ventura anamtosa Balotelli kwenye mchezo wao kati ya Lichtenstein na Ujerumani, lakini Nice walijifanya kama vipofu na kumnunua mshambuliaji huyo majira ya kiangazi.

Pamoja na mchezaji huyo, pia walimsajili Dante na Younes Belhanda, wachezaji wawili wenye uzoefu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Chipukizi Dalbert Henrique, Arnaud Lusamba na Wylan Cyprien nao walisajiliwa kuongeza ushindani kwenye kikosi hicho ambacho kina wachezaji kibao wenye vipaji. Lakini Nice iliyomaliza nafasi ya nne msimu uliopita, walimpoteza kocha wao Claude Puel majira ya kiangazi na wachezaji wao wanne.

Puel alienda Ligi Kuu England kukinoa kikosi cha Southampton, huku Hatem Ben Arfa akijiunga na PSG, Jeremy Pied (Southampton), Nampalys Mendy (Leicester) na Valere Germain (Monaco).

Lakini hiyo haijaharibu kitu kwenye kikosi chao. Favre amekuwa chaguo sahihi kuziba pengo la Puel kwa sababu anafanya vizuri na wachezaji chipukizi. Ambaye amewafanya Balotelli kung’ara akiwa na mabao hayo sita, huku mshambuliaji mwenzake Plea akitingisha nyavu mara saba na kuifanya Nice kuwa na wachezaji wawili vinara wa mabao kwenye ligi.

Kiungo Jean Seri amepika mabao sita na hakuna aliyevuruga pasi kama beki wa kati wa Malang Saar, akiwa na umri wa miaka 17.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -