Wednesday, October 28, 2020

BARBARA STREISAND: MKALI WA NYIMBO ZA MAPENZI ZENYE HISIA KALI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA NEEMA STEPHEN, TSJ


NI mwigizaji, mwimbaji, mwongozaji, mtunzi wa mashairi, mtayarishaji, msanifu, mshiriki na kiongozi wa kazi zake za kimuziki.

Kutokana na umahiri wake katika muziki, ubunifu na sanaa nyingine, amefanikiwa kutwaa tuzo nyingi zaidi ya msanii yeyote duniani kwa mujibu ya takwimu mbalimbali kama zinavyoonekana kwenye mitandao tofauti ya intaneti.

Huyo ni Barbra Streisand, ambaye kutokana na mafanikio yake aliyoyapata kupitia kazi za kimuziki na ubunifu, alifanikiwa kushinda tuzo za Oscar, Tony, Emmy, Grammy na Directors Guild of America, Golden Globe.

Pia alitwaa tuzo ya National Endowment for the Arts na ile ya Peabody, ikiwa ni pamoja na tuzo aliyopewa na Chuo cha Filamu ya Marekani ya American Film Institute’s Lifetime Achievement.

Barbra pia ni msanii pekee mwongozaji wa filamu aliyetwaa tuzo ya Kennedy Center Honors.

Alitwaa tuzo ya Oscars kama mwigizaji bora wa kike na mtunzi bora wa nyimbo, filamu tatu alizoziongoza, zilipigiwa kura ya tuzo za Oscar mara 14.

Na kichekesho chake alichoandaa hivi karibuni, kiliibuka kuwa bora kuliko vyote.

Alitengeneza albamu zilizoshika nafasi ya kwanza katika ubora kwa miongo minne mfululizo na kuwa mwanamke aliyeuza zaidi kazi zake kuliko wote.

Kutokana na mafanikio yake katika muziki, alianzisha mfuko wake wa Streisand Foundation ambao ulimwingizia Dola za Kimarekani Milioni 700.

Katika maisha yake ya muziki na sanaa, Barbra amekuwa akibebwa zaidi na ubunifu wake wa hali ya juu, ambao ndiyo uliomfanya afikie alipo sasa.

Filamu ya “The Prince of Tides” ndiyo ya kwanza kuongozwa na mwanamke, iliyomfanya atwae tuzo ya mwongozaji bora.

Tangu wakati huo, mwanamuziki huyo aliendelea kujipatia umaarufu katika kila pembe ya dunia, huku akitwaa tuzo kemkem.

Mkali huyo wa nyimbo za ‘country’ zenye uwezo wa kumtoa ‘nyoka pangoni, pia amekuwa akibebwa na sauti yake ya ajabu, nyororo, lakini ikisikika vilivyo tofauti na ilivyo kwa wanamuziki wengine, iwe ni huko Ulaya, Marekani au hata hapa Tanzania.

Albamu yake ya kwanza aliyoipa jina la “The Barbra Streisand”, ilimwezesha kutwaa tuzo mbili za Grammy mwaka 1963.

Moja ya albamu hizo, ilitwaa tuzo ya kuwa albamu ya mwaka huo; wakati huo akiwa ni msanii chipukizi kuliko wote kutwaa tuzo.

Katika upande wa sinema, alishinda tuzo ya Academy ya mwigizaji bora kupitia kazi yake ya “Funny Girl,” mwaka 1968.

Nayo kazi yake ya “Yentl” ya mwaka 1983, ilimfanya kuwa mwanamke wa kwanza kutayarisha, kuongoza, kuandika na kuwa nyota katika filamu.

Babra anashikilia rekodi ya kuwa mtayarishaji mwanamke kushinda tuzo ya Academy, hiyo ilikuwa ni kupitia wimbo wake wa “Evergreen,” ambao ulikuwa ni chombezo katika filamu yake ya mwaka 1976 iliyotikisa vilivyo katika anga la filamu ya “A Star Is Born.”

Mwaka 1997 alichaguliwa tena kuwa mtunzi bora kupitia wimbo wake wa “I Finally Found Someone”.

Kipindi chake cha kwanza cha televisheni cha “My Name Is Barbra” (1965), kilimfanya atwae tuzo ya Emmy na ile ya Peabody.

Mbali na tuzo kemkem alizotwaa mwanamama huyo, pia alipewa medali ya sanaa na Rais Bill Clinton wa Marekani, iliyopewa jina la Tuzo ya Ubinadamu, ikiwa ni katika kampeni za Haki za Binadamu.

Heshima hiyo ilifuatiwa na nyingine nyingi kutoka kwa viongozi kadhaa wa ngazi za juu serikalini, ikiwamo ya Rais wa Ufaransa mwaka huo.

Barbra, alizaliwa Aprili 24, 1942 mjini Brooklyn , Marekani, mama yake akiwa ni Diana na baba, Emanuel Streisand.

Baba yake ambaye alifariki dunia wakati Barbra akiwa na umri wa miezi 15, alikuwa ni mwalimu anayeheshimika mno.

Barbra alipata elimu yake katika shule ya Erasmus iliyopo Brooklyn, na katika maisha yake ya kimuziki, alifanikiwa kufanya shoo kadhaa katika klabu, ikiwamo ile ya Manhattan .

Kutokana na umahiri wake, aliweza kuzivutia kampuni za muziki za Bon Soir na Blue Angel, ambazo zilionyesha nia ya kuwa naye.

Alisaini mkataba wa kufanya kazi na Columbia Records mwaka 1962, na albamu yake ya kwanza iliweka rekodi ya mauzo makubwa zaidi yaliyofanywa na msanii wa kike.

Baadhi ya kazi zake alizoziandaa ni pamoja na A Piece Of Sky, Being Alive, I Believe – You’ll Never Walk Alone, I’ve Finally Found Someone, If I Could, Love Light, Memory, No Matter What Happens, No Wonder (part I), No Wonder (part II) ba No Wonder (part III).

Nyingine ni People, Places That Belong To You, More Barbra Streisand, Some Good Things, The Rose, The Way I Feel, The Way We Where, This Is One Of Those Moments, Tomorrow Night, What Kind Of Fool, What Were We Thinking Of, Where Is It Written, Will Someone Ever Look At Me That Way, Woman In Love, You And Me Always na nyingine nyingi.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -