Saturday, November 28, 2020

BARCA KUUDUWAZA TENA ULIMWENGU KWA JUVE?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

TURIN, Italia

JUZI Barcelona walikubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Juventus katika mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Huo ni mtihani mzito kwa Barca ambao watalazimika kupata ushindi wa zaidi ya mabao 3-0 pale Catalunya ili kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.

Paulo Dybala aliyetupia mawili na Giorgio Chiellini ndio walioifanya safari ya Barca kwenda nusu fainali kuwa ngumu pindi timu hizo zitakaporudiana Aprili 19.

Hata hivyo, huenda historia nzuri waliyonayo Juve kwenye uwanja wao wa nyumbani ilikuwa chanzo cha Barca kupoteza mchezo wa juzi.

Kabla ya kukutana Juve hawakuwa wamefungwa katika michezo 47 ya michuano mbalimbali iliyochezwa uwanjani hapo.

Kwa mara ya mwisho Juve kufungwa katika uwanja huo, walipokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Bayern Munich na hiyo ilikuwa katika msimu wa 2012-13.

Itakumbukwa kuwa, mwezi uliopita Barcelona waliushangaza ulimwengu wa soka kwa kuifunga PSG jumla ya mabao 6-5, ikiwa ni baada ya kufungwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa Ufaransa.

Baada ya kufungwa mabao 4-0,  ilionekana kuwa safari ya Barca ingeishia hatua ya 16 bora, lakini walishinda mabao 6-1 katika mchezo wa pili.

Hata hivyo, juzi Barca hawakuwa kwenye ubora waliouonyesha katika mchezo wa marudiano dhidi ya PSG. Kasi ya Juve na mabao mawili ya kipindi cha kwanza ya Dybala yalionekana kuwamaliza kabisa Wacatalunya hao.

Lakini pia safu ya ulinzi ya Juve iliyokuwa chini ya mlinda mlango mkongwe, Gigi Buffon, mabeki Chiellini, Leonardo Bonucci na Alex Sandro ilifanikiwa kuzima makali ya washambuliaji wa Barca.

Neymar ambaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu dhidi ya Malaga, hakuweza kuonyesha makali yake mbele ya walinzi hao.

Kwa kipindi chote cha dakika 90 za mchezo, nyota huyo wa zamani wa Santos hakupiga hata shuti moja lililolenga lango.

Kama ilivyo kwa Lionel Messi na Luis Suarez, mara nyingi alijikuta akichafuliwa upepo na Chiellini na Bonucci. Mabeki hao wameonekana kujenga ukuta imara msimu huu ambapo wameruhusu nyavu zao kutikiswa mara mbili pekee.

Nicolas Pareja wa Sevilla na Corentin Tolisso anayeichezea Lyon ndio wachezaji pekee waliomfunga kipa Buffon katika michuano ya mwaka huu.

Tatizo la mabeki lilionekana pia wakati kikosi hicho kilipochapwa na Deportivo La Coruna katika mchezo wa La Liga kabla ya kuwafunga Valencia.

Kulingana na takwimu zao za hivi karibuni, ni wazi Barca watakuwa na kazi kubwa ya kupindua matokeo ya juzi.

Dhidi ya Juve, ilikuwa ni mechi yao ya pili kushindwa kufunga bao huku safu ya ulinzi ikionekana kuwa dhaifu.

Barca walionekana wazi kumkosa Dani Alves kwenye eneo la beki wa pembeni. Akiwa na Juve juzi, Alves alikuwa kizingiti kwa washambuliaji wa Barca.

Sergi Roberto wa barca hakuweza kufanya kazi nzuri kwa upande wa winga wa kulia, nafasi ambayo Alves alikuwa akiicheza kwa ustadi mkubwa akiwa Catalunya.

Kumchezesha Jeremy Mathieu ambaye aliboronga mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Malaga na kukosekana kwa Sergio Busquets, ilikuwa tatizo jingine kwa upande wa Barca.

Javier Mascherano aliyechukua nafasi ya Busquets katika eneo la kiungo, alifunikwa na Wafaransa hao. Licha ya Juve kuwaachia Barca wamiliki mpira, bado wakali hao wa La Liga hawakuwa na madhara.

Neymar hakupewa nafasi ya kupumua na Mrazil mwenzake, Alves ambaye aliwahi pia kucheza naye Barca.

Beki Mathieu hakuweza kumzuia winga Cuadrado kupandisha mashambulizi.

Keshokutwa siku nne kabla ya timu hizo kurudiana, Juve watashuka dimbani kumenyana na Pescara na Barca watakuwa wakivaana na Real Sociedad.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -