Tuesday, October 27, 2020

Barnaba, Sheta, Ben Pol wafunika Fiesta Tanga

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA MWANDISHI WETU, TANGA

BAADA ya kuchengua mikoa ya Dodoma na Morogoro, Tamasha la Tigo Fiesta mwishoni mwa wiki lilihamishia burudani yake mkoani Tanga  ambapo kama kawaida wasanii walipanda jukwaani na kuporomosha burudani ya uhakika kwa maelfu ya mashabiki waliojitokeza kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Tamasha hilo la kila mwaka ambapo huendeshwa na Kampuni ya PrimeTime Promotion chini ya Clouds Media mwaka huu linadhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo chini ya kaulimbiu ya Imoo ambapo pamoja na burudani, lakini pia kampuni ya Tigo imekuwa ikitoa misaada mbalimbali ikiwemo kuchangia madawati kwenye shule katika baadhi ya maeneo tamasha hilo linakofanyika.

Katika tamasha la Tanga, wasanii Elias Barnaba, Sheta, Ney wa Mitego na Ben Pol ni baadhi tu ya wasanii mahiri walioshambulia jukwaa katika Uwanja wa CCM Mkwakwani na kukonga nyoyo za mashabiki wengi waliojitokeza kupata burudani.

Burudani iliyoporomoshwa na wasanii katika tamasha hilo iliacha historia ya aina yake hasa kutokana na ukweli kwamba wasanii wengi walijimwaga kuimba nyimbo zao mpya na zamani huku kila mmoja akitaka kufanya vizuri kumfunika mwenzake hali ambayo ilisababisha tamasha hilo kunoga kwa kila aliyepanda jukwaani kujituma akiogopa kufunikwa.

Wasanii wengine waliopagawisha katika tamasha hilo ni pamoja na Roma Mkatoliki, Makomando, Dogo Janja, Snura pamoja na Matonya ambao walifanya shoo kabambe zilizowapagawisha mashabiki wa muziki wa Jiji la Tanga.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -