Saturday, November 28, 2020

BAYERN KUMBE NDIYE BINGWA UEFA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali inaanza leo, ambapo itashuhudiwa miamba nane ikiumana kusaka tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali.

Miamba ambayo itashuka viwanja tofauti ni Juventus, ambao leo  watakuwa wenyeji wa FC Barcelona na AS Monaco, ambao watakuwa ugenini nchini Ujerumani kuikabili na huku kesho kukiwapo mtanange ambao unatajwa kuwa kama fainali kati ya Bayern Munich na Real Madrid utakaopigwa katika Uwanja wa Allianz Arena.

Mechi nyingine itakuwa ni kati ya Atletico Madrid ambao watawakaribisha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Leicester City, kwenye uwanja wao wa Vicente Calderon.

Kutokana na ushindani na ubora wa vikosi vilivyofanikiwa kutinga hatua hiyo, yamekuwa yakizungumzwa mengi kuhusu ni nani atakayefanikiwa kuvuka hatua hiyo na kutinga nusu fainali na hata kutwaa ubingwa.

Ni katika mabishano hayo ambapo kila mpenda soka amekuwa akiitabiria timu gani itaibuka kidume na ipi ambayo itaweza kuangukia pua.

Hata hivyo, BINGWA baada ya kupitia chambuzi za wadau mbalimbali wa soka imebaini kuwa Bayern Munich ndiyo inapewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo.

Katika chambuzi hizo wadau hao wanadai kuwa licha ya mabingwa hao wa Ligi ya  Bundesliga kuanza kwa kusuasua mwanzoni mwa michuano hiyo ya UEFA, lakini baadaye chini ya kocha wao, Carlo Ancelotti, walizinduka katika hatua ya 16 na kutembeza kipigo cha mbwa mwitu kwa   Arsenal.

Kabla ya kupata ushindi huo, mabingwa hao wa Ujerumani walianza kuchanganya gia katika hatua ya makundi ambapo waliweza kufuzu wakiwa na mechi mbili mkononi, licha ya kupoteza mchezo mmoja kwa bao 1-0 walilofungwa na Atletico Madrid.

Kipigo hicho kilifuatiwa na kingine cha mabao  3-2 kutoka kwa Rostov, jambo ambalo liliwafanya mashabiki wengi kudai kuwa kikosi hicho ni dhaifu, lakini kitendo cha kuifunga Arsenal jumla ya mabao 10-2 ndicho kilichomaliza fikra hizo.

Katika rekodi yao msimu huu, vinara hao wamecheza mechi nane na kushinda sita, hawajatoka sare, wamepoteza miwili, wamefunga mabao 24 na wameruhusu nane.

*Jinsi Bayern walivyotinga nane bora

Pamoja na kuwa na mafanikio makubwa katika miaka ya hivi karibuni, kiwango cha   Bayern katika safari za mechi zake barani Ulaya hakikuwa kizuri wakati wenzao wakitakata.

Hali hiyo ni kutokana na kwamba wakati Novemba mwaka jana ikisafiri kwenda kuivaa  Eindhoven ilikuwa haijawahi kupata ushindi ikiwa ugenini katika kipindi cha miezi 11 na ilionekana ingeendelea kuandamwa na balaa hilo, baada ya kujikuta ikitangulia kufungwa, lakini mabao mawili yaliyofungwa na Robert Lewandowski  yakaondoa mkosi huo kabla ya  ushindi wa  5-1 dhidi ya Arsenal kuwahakikishia nafasi hiyo.

*Kwa nini huu ni mwaka wa Bayern

Kuna kila sababu pamoja na matatizo yote yaliyowahi kuwakumba  Bayern katika mechi za ugenini, lakini walifanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano hiyo mara tatu kutokana na kurekebisha makosa yao walipokuwa wakicheza mjini Munich.

Kipindi hicho pia kilikuja ikiwa ni baada ya miaka mitatu napo wakishindwa kufanya vizuri katika mechi za nyumbani za michuano hiyo ya  UEFA, lakini wakawa wabaya walipokuwa wakicheza ugenini, jambo ambalo wameanza kuonekana kuwa nalo tena kwa sasa na hivyo inaweza kuwa vigumu kuwafunga  hata wakiwa ugenini.

*Takwimu muhimu katika mechi yao ya kesho dhidi ya Real Madrid.

Klabu hizo zinaonekana kuwahi kukutana mara  22 katika michuano yote ambapo  Bayern waliweza kushinda mara 11, wakalazimisha sare mara mbili, wakapoteza tisa na kati ya mechi hizo walizoshinda wakiwa nyumbani ni tisa sare mbili na wakapoteza mmoja.

*Anayeweza kuwapa taji hilo

Straika Robert Lewandowski ndiye aliyebeba taji hilo mikononi mwake. Kutokana na kuwa kinara huyo wa timu ya Taifa ya Poland, msimu uliopita ndiye aliyeifungia timu hiyo mabao 42 na anavyoonekana kwa sasa yupo mbioni kuzidi    idadi hiyo.

Hadi sasa staa huyo ameshaichezea Bayern Munich mechi 17 za michuano hiyo ya 17 na kati ya hizo ameiwezesha timu hiyo kushinda 16.

*Nyota wanaokuja juu: Joshua Kimmich, staa huyo ni mbadala wa muda mrefu wa  Philipp Lahm kwa klabu hiyo na taifa lake.

Akiwa na umri wa miaka 22, tayari nyota huyo ameshaonesha makali yake kwa vikosi hivyo viwili kutokana na uwezo wake wa kumudu nafasi za beki wa kulia, kati ama kiungo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -