Wednesday, October 21, 2020

BEKI KISIKI AWAITA SIMBA MEZANI

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA ZAITUNI KIBWANA


BEKI kisiki, Salum Kimenya, amewaita mezani Simba ili kujadiliana naye juu ya  dau la uhamisho wake kutoka kikosi cha Tanzania Prisons anachokitumikia.

Kimenya ambaye ni kiboko ya Simba kutokana na jinsi alivyowadhibiti katika mechi ya mzunguko wa kwanza, amesema wazi kwamba hana pingamizi la kujiunga na timu hiyo kama watafikia makubaliano na kumlipa dau analolitaka.

Beki huyo si mara ya kwanza kutakiwa na Simba, anakumbukwa na mengi na mabosi hao, baada ya kusimamia vema eneo la ulinzi pale kikosi chake cha Tanzania Prison kilipovaana na Simba na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Akizungumza na BINGWA, Kimenya kwa sasa hakuna kinachomzuia kutua kwenye kikosi hicho, lakini suala nzima la dau limekuwa likimkwamisha hasa baada ya vigogo hao kuwasilisha mezani dao dogo ambalo alilitaja kutoendana na hadhi yake.

“Siwezi kusaini kwa dau dogo kama lile wanalolitaka Simba, kama wananiamini na kutambua uwezo wangu basi waongeze dau ili nimalizane nao,” alisema

Alisema awali Simba walitaka kumpa milioni 20, dau ambalo aliligomea lakini mpaka sasa vigogo hao bado wameshikilia msimamo wao ule ule.

“Simba walifanya mazungumzo na mama na wakaniambia nimalizane nao, cha ajabu wanataja dau lile lile la awali ambalo nililigomea,” alisema.

Kimenya anayekipiga kwenye kikosi cha Tanzania Prisons, ni beki kisiki kwenye timu hiyo na mwenye uwezo wa kuamini anahitajika na Simba katika kuongeza nguvu safu ya ulinzi ya timu hiyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -