PARIS, Ufaransa
BEKI wa timu ya Paris Saint Germains (PSG), Serge Aurier, amehukumiwa kwenda jela miezi miwili baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumshambulia Ofisa wa Kikosi cha Usalama Barabarani.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, alitenda kosa hili Mei mwaka huu, baada ya kutakiwa kushuka kwenye gari ili akapimwe.
Hata hivyo, Aurier ambaye anadaiwa kumpiga kiwiko kifuani ofisa huyo, anadai kushambuliwa na ofisa huyo na kusema atakata rufaa ili kupinga uamuzi wa mahakama hiyo.
“Zilikuwa ni vurugu,” Aurier alieleza katika mahojiano na kituo cha televisheni nchini Ufaransa.
“Maofisa wa polisi walitoka nje ya gari lao wakanishambulia, wakanichubua na mdomo wangu ulipata majeraha,” aliongeza staa huyo.