Thursday, November 26, 2020

Bella afanya bonge la shoo Dynasty Beach Resort

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MWANDISHI WETU

MKALI wa muziki wa dansi nchini, Christian  Bella ‘King of Melody’, amefanya shoo bab kubwa katika tukio la usiku uliopewa jina la Full Moon Party  kwenye Hoteli ya Dynasty Beach Resort iliyopo Ununio, jijini Dar es Salaam.

Shoo hiyo ilifanyika juzi Jumamosi na kuhudhuriwa na wapenzi lukuki wa burudani kutoka maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, huku ikipambwa na washiriki wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2020.

Bella akiwa na bendi yake ya Malaika, waliimba nyimba zao zote kali, kuanzia zile za zamani hadi za sasa na hivyo kukonga nyoyo za mashabiki waliojitokeza usiku huo.

Akizungumza na Papaso la Burudani jana, Mkurugenzi wa Dynasty Beach Resort, waandaaji wa onyesho hilo,  Manase Mwakale, alisema kuwa amefarijika kuona wapenzi wa burudani waliojitokeza wakikatwa kiu na Bella na wanamuziki wenzake wa Malaika.

“Daynas  tumepanga kukuza utalii wa nchi yetu kwa njia ya fukwe zetu ndiyo sababu ya kuandaa Full Moon Party  ambayo imekuwa ikifanyika nchi za wenzetu na kuleta maendeleo makubwa,” alisema Mwakale.

Alisema kutokana na mwitikio wa watu wakliojitokeza juzi, wamepanga kuendelea kuandaa maonyesho mbalimbali ili kuwapa burudani wateja wao na wadau wa saa hiyo kwa ujumla.

Mbali ya burudani, Mwakale alisema kila wikiendi watakuwa wakionyesha mechi mbalimbali za soka, kuanzia zile za Ligi Kuu Tanzania Bara hadi za Ulaya, hivyo kuwataka wapenzi wa mchezo huo, kujumuika na wenzao huko.

“Wapenzi wa soka hatujawasahau, wasisite kuja Dynasty Beach Resort kila wikiendi kwani pamoja na burudani ya muziki, tutakuwa tukionyesha mechi za soka za ligi mbalimbali, zikiwamo za Ulaya kupitia ‘screen’ kubwa zilizopo hapa Dynasty,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -