Friday, December 4, 2020

BEN POL ALIVYOWAROGA WAREMBO DAR KWA MKWANJA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA KYALAA SEHEYE,

STAA wa Bongo Fleva, Benard Paul ‘Ben Pol’, ameonyesha jeuri ya fedha baada ya kununua kopi ya filamu ya Single Ziro kwa Sh 150,000 wakati wa uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa Aqua uliopo Coco Beach, jijini Dar es Salaam.

Filamu hiyo ni mali ya msanii, Hisani Muya ‘Tino’ ambayo imetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu.

Ben Pol kwa sasa anadhaminiwa na Kampuni ya Magita Investment inayojishughulisha na uuzaji wa magari, nyumba, mikopo kwa watu wote na kutoa huduma za bima za aina mbalimbali hapa nchini, lakini pia ikiwa na shule ya kufundishia udereva.

Mara baada ya kununua filamu hiyo, wapenzi wa burudani waliofurika kwenye ukumbi huo hasa ‘warembo wa mjini’, walionekana kupagawa na msanii huyo kwa jeuri yake hiyo ya fedha aliyoionyesha.

Akizungumza na BINGWA juzi, Ben Pol alisema yeye kama mwanamuziki ni lazima asapoti filamu za nyumbani kwa kuwa wanategemeana, hivyo haifai kuonyeshana dharau kwa sababu wanafanya kazi inayofanana.

“Ukiwa mwanamuziki inakupasa umsapoti kila msanii bila kuangalia sanaa yake, kwani nikishirikiana na Tino nina imani mashabiki wake watapenda kazi yangu na sanaa ndivyo inavyotaka, si kuonyeshana dharau na ubabe,” alisema Ben Pol.

Aidha, alifafanua kuwa mbali na kumsapoti kama msanii pia ni mwanafamilia mwenzake chini ya Kampuni ya Magita.

Ukiachana na Ben Pol, Mkurugenzi wa Magita Investment, Samwel Magita, naye alifanya kweli kwa kununua kopi moja ya filamu hiyo kwa Dola za Marekani 5,000 (Sh mil 10.9), huku msanii Daud Duma na Meneja Maneno wakinunua kopi moja kwa Sh 50,000.

Uzinduzi huo ulipambwa na wasanii mbalimbali ila wasanii wanaounda kundi la Pah One ambao wamemaliza bifu lao na Navy Kenzo hivi karibuni, waliwapagawisha na kuwachezesha vyema mashabiki pamoja na mastaa wenzao.

Pah One waliweza kuwanyanyua Ben Branko  ‘Segerengo’, Ben Pol, Tino, JK Komedian, Duma na wengine wengi baada ya kupanda jukwaani na kuanza kushusha ngoma zao kali na hivyo ukumbi mzima ukalipuka kwa shangwe.

Naye msanii Tino ambaye aliongozana na mkewe, Otiliya Muya, alishindwa kujizuia kwa kutokuamini kama kazi yake ya Single Ziro imeweza kukusanya mashabiki lukuki kiasi kile.

“Sijui niseme nini, ila sina cha zaidi ya kusema kweli Single Ziro ilistahili kupata tuzo nchini Marekani, watu hawajaiona ila wameitikia kwa wingi sana, pia nawashukuru wasanii wenzangu walionunua filamu yangu kwa bei kubwa wakionyesha sapoti,” alisema Tino.

Tino alisema baada ya kukaa kwenye tasnia kwa miaka 19, filamu hiyo ndiyo imempa mafanikio makubwa na sasa anageukia filamu za ‘Action’ akiamini huko ndiko sehemu sahihi kwake.

“Niko mwenye ‘game’ miaka 19, nimeshafanya filamu nyingi sana ila nimegundua filamu za mapigano ndizo hasa zinanilipa na kuniweka katika ramani nzuri kwenye soko la filamu japokuwa wakati naanza kuigiza, waongozaji wengi waliniweka kwenye filamu za mapenzi,” alisema Tino.

Aliwaasa wasanii wenzake wenye ndoto za kufanya filamu za mapigano ambao hawajui kupigana, wafanye mazoezi mwisho wa siku wataweza tu.

Katika hatua nyingine, Magita kupitia kampuni yake ya Magita Investment, wametangaza rasmi kumdhamini Tino na  Ben Pol ili waweze kufanya kazi zao bila msongo wa mawazo wakijua kabisa hawana shida yoyote.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -