Tuesday, October 27, 2020

BEN POL: NITAMUOA MWANAMKE ATAKAYEKUWA MBELE YANGU

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

 

KARIBU msomaji wa Jiachie na Staa Wako, inayokukutanisha na mastaa uwapendao. Leo tupo na Benard Paul ‘Ben Pol’ ambaye ni nyota wa Bongo Fleva, anayefanya vizuri na wimbo Amen alioshirikishwa na Maua Sama, karibu.

SWALI: Imma wa Kurasini, Dar es Salaam anauliza kwanini uliamua kuweka nywele zako rangi ya kijani?

Ben Pol: Kwa sababu ni rangi ambayo haijazoeleka sababu nilitaka kuwa na mwonekano tofauti lakini pia nilijiona kama msanii, nina jukumu la kutunza mazingira na ninashukuru ilikuwa na ‘impact’ kwenye jamii lakini sasa hivi nimeziondoa kabisa nipo kama zamani.

SWALI: Mustafa Rengo wa Butiama, anauliza ilikuchukua muda gani kumsimamia msanii Wyse kimuziki na vigezo gani ulivitumia?

Ben Pol: Mimi ni mtu ambaye natumia zaidi hisia kugundua kipaji cha mtu, moyo na masikio yangu huwa havinidanganyi, nilikutana naye Dodoma alikuwa anaimba, nikatambua uwezo wake ndiyo ikawa hivyo, nashukuru anaendelea vizuri kuanzia kwenye wimbo wangu Bado Kidogo, Siamini na sasa ana ngoma yake.

Kikubwa tupeane sapoti kwa sababu kupitia ‘Ben Pol Present’, vijana wengi wataendelea kunufaika, muziki ni mkubwa lazima tusaidiane wote tupate ugali, mpango wangu huu ni endelevu wa kuinua vipaji popote pale nitakapokutana navyo.

SWALI:  Justine Bulinda wa Vingunguti Dar es Salaam, anauliza muziki gani ambao hausikilizi?

Ben Pol: Mimi nasikiliza muziki wa aina yoyote ile kuanzia Zilipendwa, Mnanda, Singeli, hip hop, bolingo, gospo hadi taarabu tena nawashangaa sana ambao wanasema hawasikilizi taarabu wakati maneno ni yale yale yanayotumika kwenye miziki mingine.

SWALI: Faiza Mahmood kutoka Tanga, anauliza ongezeko la mastaa wenzako ambao ni marafiki zako wanaoa je, wewe hawakushawishi kufanya hivyo?

Ben Pol: Inanigusa kwa namna moja ama nyingine, ila naamini itafika siku na mimi nitaoa. Huo muda ukifika nitaoa mwanamke atakayekuwa mbele yangu kwa sababu huwa siangalii historia za mapenzi ya nyuma kwamba umetoka wapi na mtu ambaye unamuoa.

SWALI: Aneth Lundela wa Mtwara, anauliza wewe ni mtu wa aina gani na unapenda kufanya nini ukiwa nyumbani?

Ben Pol: Mimi ni mtu wa kawaida, napenda marafiki wapya, napenda kutoka, kusikiliza muziki, kusoma mambo tofauti tofauti na nikiwa nyumbani nikaamka asubuhi nikakosa cha kufanya napenda kufanya komedi.

SWALI: Mzela wa Mbezi, Dar es Salaaam, anauliza baada ya kutoa wimbo na Kiss Daniel je, kolabo gani mashabiki zako tusubirie?

Ben Pol: Zipo nyingi ambazo nyingine tayari zimetoka kama vile ile niliyofanya na Butela wa Rwanda, Otile Brown na King Kaka wa Kenya, kuna UG na MzVee wa Ghana na nyingine nyingi ambazo nimefanya zipo tu ndani nasubiri muda ufike.

SWALI: Izack Mchome wa Iringa, anauliza wewe ni rafiki wa msanii Darasa. Je, ni kweli anatumia dawa za kulevya ndiyo maana amepotea?

Ben Pol: Hapana siamini kama anatumia dawa za kulevya, sababu sina ishara yoyote ambayo nimeiona kwake, tunaongea kila siku kwenye simu saa zima, yupo poa sana hana tatizo lolote.

SWALI: Wasanii gani wa nje walikuvutia mpaka ukajikita katika kufanya muziki wa RnB?

Ben Pol: Baby Face, Boys 2 Men, Maxweel, R Kelly, Eric Wainaina na wengine wengi.

SWALI: Rachel Stanford anauliza msichana wa aina gani unaweza kuwa naye kwenye uhusiano?

Ben Pol: Awe na akili ‘smart’, mchangamfu na anaongea sana maana mimi siongei sana kwa hiyo tutaendana, awe na ‘confidence’ (jasiri) na kujitambua.

Wiki ijayo tutakuwa na rapa Wakazi, tuma swali lako kwake kupitia namba hapo juu.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -