Friday, October 23, 2020

Ben Pol: “Snura alini-kiss” kama kunipa sapoti tu

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA BEATRICE KAIZA,

Swali: Elly Patrik wa Muheza, Tanga, kaka Ben Pol mbona sijawahi kumsikia mpenzi wako au wewe hauna mpenzi na kama unaye anaitwa nani?

Jibu: Nina mpenzi ila mara nyingi huwa napenda kuweka mambo binafsi chini ya kapeti, hususani mambo ambayo hayahusiani na muziki.

Swali: Naitwa Juster nipo Dar es Salaam, napenda sana nyimbo zako, lakini nataka kujua umejipangaje kuufikisha muziki kimataifa?

Jibu: Kila kitu ni hatua kwa hatua, nina kolabo na msanii wa nje, muda mwafaka ukifika nitaachia, pia tayari baadhi ya kazi zangu zinachezwa kwenye vituo vya kimataifa.

Swali: Pongezi kwenu BINGWA kwa mambo mazuri mnayotufanyia, swali langu kwa Ben Pol, ana watoto wangapi na je, amefunga ndoa au bado? Pia vipi suala la ibada anaenda kanisani maana wasanii wengi hawafanyi ibada, jina langu ni Othuman kutoka Dodoma, Tanzania.

Jibu: Nina mtoto mmoja anaitwa Mali, huwa nasali mara nyingi peke yangu au na familia yangu, pia naenda kanisani japo si mara nyingi kutokana na safari za kikazi kuwa nyingi.

Swali: Naitwa Mack the Don, nipo pande za Sakina Arusha, kiukweli naukubali muziki wako uko vizuri japo mimi ni mwana hip hop, wewe na Ali Kiba mnatisha, huwa nafuatilia sana kazi zenu big up kaka.

Jibu: Asante sana Mack the Don kwa kukubali kazi zangu na za Ali Kiba, tupo pamoja sana watu wangu wa Arusha.

Swali: Neema Anderson wa Tegeta, Dar es Salaam, kaka yangu upo juu sana una utunzi wa kitofauti katika kazi zako na pia wewe una sauti nzuri ya kuimba nyimbo za gospel ‘injili’, nakumbuka kuna siku uliimba na Clement Paul, mlipendeza sana toa hata gospel.

Jibu: Nashukuru sana Neema nikipata kitu kizuri ambacho kinahusiana na gospel nitatoa, asante kwa ushauri mzuri.

Swali: Ally Mussa wa Kibaha, namkubali Ben Pol, anajua kuimba na pia ni msanii ambaye hana skendo chafu kama wasanii wengine, swali langu kwake yeye kama kwa uwezo wake alionao wakuimba ni msanii gani wa kiume anayemkubali zaidi hapa Tanzania.

Jibu: Wasanii wa kiume ambao ninawakubali ni wengi sana hapa Tanzania, kuna Barnaba, Belle 9, Jux, G Nako, yaani wapo wengi kusema ukweli hao ni wachache ambao naweza kuwataja kwa haraka haraka.

Swali: Marth a.k.a Kim Nana, nampenda sana Ben Pol namshauri akaze kwenye muziki kwani wasanii wamekuwa wengi.

Jibu: Sawa asante kwa ushauri mzuri Marth Kim Nana, nitafanya hivyo.

Swali: Naitwa Idi Mrisho wa Tabora, nataka kufahamu ulianza kuimba muziki mwaka gani?

Jibu: Nilianza kupenda muziki tangu nilipokuwa na miaka mitano, hiyo ilikuwa mwaka 1994, rasmi nilikuwa msanii mwaka 2007.

Swali: Naitwa Muyuga nipo Bunda ni kolabo gani ya kimataifa tutegemee mashabiki zako na ngoma gani inayofuata kwa sasa?

Jibu: Kolabo za kimataifa nimefanya nyingi sana na nimefanya na watu wengi, ngoma inayofuata ikiwa tayari nitasema hata kwenye mitandao ya kijamii huwa naweka kama nina nyimbo mpya.

Swali: Subira Said wa Tanga, kwanini umesema hutafanya shoo tena hadi Desemba, una matatizo gani?

Jibu: Subira sijasema kama sitaki kufanya tena shoo hapana, ila nimesema kwa sasa siwezi kufanya shoo hadi Desemba kwa kuwa ratiba yangu tayari iko bize.

Swali: Michael Nelson wa Korogwe, Tanga. Swali langu kwa Ben Pol, lini atakuja kufanya shoo Tanga maana shabiki zake tunamhitaji tuongee naye japo kwa ufupi?

Jibu: Sawa Nelson nakuja Tanga muda si mrefu kufanya shoo, mashabiki zangu msijali kaeni mkao wa kula watu wangu wa nguvu Tanga.

Swali: Father Amasha wa Igundu, Chunya. Mimi ni shabiki wa Ben Pol namba moja napenda sana muziki wako, je, una malengo ya kusaidia vijana wa Dodoma kimuziki. Pia naipenda sana singo yako ya maneno maneno.

Jibu: Yeah! Vijana wa Dodoma tupo pamoja kusaidiana ni muhimu sana, msijali nashukuru sana kwa kupenda nyimbo yangu ya maneno maneno.

Swali: Gladness Samwel wa Arusha. Ni kweli wewe na Snura ni wapenzi? Na kama si wapenzi kwanini mlibusiana mbele za watu kwenye tamasha la Fiesta mkoani Tabora?

Jibu: Snura ni rafiki yangu tu hakuna kitu  kinachoendelea, kuhusu kunikiss alikuja kunipa sapoti tu.

Swali: Dada Beatrice, asante sana kwa kutupa nafasi sisi wasomaji ili tuweze kutoa ya moyoni na kujua vitu mbalimbali vya wasanii wetu wa hapa Tanzania, swali langu kwa Ben Pol, kwanini hufanyi kolabo na Jux, nyinyi ni wakali katika tasnia hii ya muziki wa Bongo Fleva.

Jibu: Asante kwa kutupenda na sisi tunawapenda sana mashabiki zetu, kuhusu kufanya ngoma na Jux mbona nimeshafanya naye.

Swali: Edita Emanueli wa Arusha, kwanini ulimpa mwanao jina la Mali na nini maana halisi ya jina hilo na jina la pili ni nani?

Jibu: Nimempa jina mwanangu wa kwanza jina hilo la Mali kwa sababu ni kuonyesha thamani kwa kuwa wanasema majina yanaumba. Kwa hiyo kumuita Mali ni njia ya kumtabiria mambo mema katika maisha yake.

Jina la pili la mwanangu ni Magufuli, pia nimempa jina hilo kwa sababu amezaliwa kipindi ambacho Rais Magufuli anaongoza.

Hawa ni baadhi ya mashabiki wa msanii wa Bongo Fleva, Bernard Paul ‘Ben Pol’, waliojitokeza kumuuliza maswali na hayo ndiyo majibu yake.

Wiki ijayo tunamleta kwenu msanii wa Bongo Fleva, Shilole ‘Shishi Baby’, muulize swali lolote au mpe ushauri na utume kwa kutuma sms kwenye namba iliyopo hapo juu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -