Wednesday, October 28, 2020

BENTEKE UKIMSAJILI TU, IMEKULA KWAKO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

KIBONGO bongo, Christian Benteke, angesugua sana kwenye mechi za mtaani, hakuna kocha wa ligi kuu ambaye angekuwa na ujasiri wa kumsajili. Unajua kwanini?

Katika timu tatu zote ambazo straika huyu wa Ubelgiji amezichezea, makocha waliomsajili vibarua vyao viliota nyasi.

Benteke alijiunga na Aston Villa mwaka 2012, kisha akahamia Liverpool miaka mitatu baadaye na sasa anakipiga katika klabu ya Crystal Palace alikojiunga msimu uliopita.

Katika klabu zote hizo alizopita, Benteke amekuwa na mafanikio makubwa licha ya kuwa na mkosi wa kufukuzisha kazi makocha wote wanaomsajili.

Makala haya yamekuandalia orodha ya makocha watatu ambao walijikuta wakitupiwa virago baada ya kumsajili mkali huyu anayesifika kwa mabao ya vichwa.

Paul Lambert

Lambert alikuwa kocha wa kwanza kumleta Benteke kwenye Premier League, akimsajili kwa dau la pauni mil 7 kutoka katika klabu ya Genk ya Ubelgiji.

Dili hilo lililofanyika Agosti 2012, lilikuwa na faida kubwa kwa Villa ambapo katika msimu wake wa kwanza Benteke alifunga mabao 23 na msimu uliofuata kufunga 11 baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza majeraha ya goti.

Benteke alijikuta kwenye maisha magumu zaidi akiwa Villa Park msimu wa 2014-15, ambapo klabu hiyo ilikamata nafasi ya 18 kwenye msimamo wa EPL hali iliyopelekea kocha Paul Lambert kutimuliwa kazi Februari 2015.

Baada ya Tim Sherwood kupewa kazi ya kuinoa Palace, Benteke alirudi kwenye ubora wake akifunga mabao 11 kwenye mechi 9 za kwanza alizoziongoza Sherwood.

Brendan Rodgers

Liverpool walilipa pauni mil 32.5 na kumsajili Benteke Julai 2015 na kumfanya kuwa mchezaji wa pili ghali zaidi katika kikosi chao.

Na ilimchukua michezo 10 tu mpaka Oktoba, Rodgers akatimuliwa kazi baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya mahasimu wao wa jiji, Everton na kuiacha Liverpool kwenye nafasi ya 10 katika msimamo wa Premier League.

Akiwa Liverpool, Benteke alifanikiwa kufunga mabao 10 tu katika michezo 42 aliyocheza.

Alan Pardew

Benteke hakuwa na maisha mazuri sana pale Anfield, msimu mmoja tu akawa sokoni tena na safari hii ni Alan Pardew aliyejivika mabomu na kumsajili.

Akatua kwa mbwembwe Selhurst Park na kufanikiwa kufunga mabao nane kwenye mechi 15 alizocheza, lakini hayakuwa na faida kwa Palace ambao wanashika nafasi ya 17 kwenye msimamo wa Premier League.

Kutokana na timu hiyo kuonekana kupoteza mwelekeo, uongozi ukachukua maamuzi magumu ya kumtimua Alan Pardew aliyemsajili Benteke mwanzoni mwa msimu.

“Ningependa kuchukua nafasi hii kuwashukuru watu wote wa hapa Palace kwa ushirikiano wao waliotuonyesha,” alisema Pardew. “Shukrani zangu za dhati ziende kwa wachezaji wangu na mabosi wetu wakiongozwa na Steve Parish, tumekuwa pamoja katika nyakati zote.

“Binafsi nimevutiwa sana na mazingira ya klabu hii na ninasikitishwa sana kwa hiki kilichotokea, ni mambo ya kawaida kabisa kwenye soka.

“Naamini klabu haitayumba wala kuathirika na lolote kwa kuondoka kwangu, niwatakie kila la kheri wote ambao watabaki hapa na kuendelea kuipigania klabu hii kutimiza malengo tuliyojiwekea.

“Kwa sasa sina la kuongeza, nahisi muda wangu wa kukaa hapa umeisha na natakiwa kuanza maisha mapya, ” alimaliza Pardew.

Je, mkosi huu wa Benteke kufukuzisha kazi makocha utaendelea mpaka lini? Hakuna mwenye majibu ila kwa wakati huu Palace wako kwenye mazungumzo na Sam Allardyce kwa ajili ya kuziba nafasi iliyoachwa na Pardew.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -