Friday, January 15, 2021

Bhinda: Kinachoitesa Simba ni bao 5-0 walizofunga 2011/12

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA GRACE HOKA

NDANI ya klabu za soka za Simba, Yanga na nyinginezo, kuna watu ambao wamekuwa na mchango mkubwa, lakini wakionekana kusahaulika kadri siku zinavyokwenda.

Kwa kutambua hilo, BINGWA tumeanzisha safu hii ambayo itakuwa inawaletea viongozi au wanachama maarufu wa klabu za soka na michezo mingineyo ambao waliwahi kufanya mambo makubwa siku za nyuma.

Leo aliyepata fursa ya kuizindua safu hii ni mwanachama maarufu wa Yanga, Mohammed Bhinda.

Katika mahojiano na BINGWA hivi karibuni, pamoja na mambo mengine, Bhinda anasimulia tukio ambalo ataendelea kulikumbuka maishani mwake: “Toka nilipoanza kuipenda Yanga nikiwa shabiki, meneja na mjumbe wa kamati ya utendani, hakuna siku niliyoumia kama tulipofungwa na Simba  mabao 5-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa  2011/12 kwenye Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru), Dar es Salaam.

“Ilikuwa ni siku ya majonzi kwangu, siku ile niliumia sana, nilikuwa jukwaa kuu nikiona Yanga ikitandikwa mabao matano, wakati tunafungwa hayo mabao, mwenyekiti wa Simba alikuwa  Ismail Aden Rage, wakati makamu wake alikuwa ni Geoffrey  Nyange ‘Kaburu’.”

Wakati Yanga inafungwa mabao hayo 5-0, Bhinda alikuwa ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga, ambapo kabla ya kuwa na wadhifa huo, aliwahi kuwa meneja wa timu hiyo.

“Kilichoniuma hadi hii leo ni kwamba, sisi wenyewe Yanga ndio tulitengeneza mpango wa kufungwa yale mabao kwa sababu ya chuki kwa mwenyekiti wetu wakati huo, Lloyd Nchunga, ambapo kuna baadhi ya wanachama walikuwa wakitaka aondoke madarakani,” anasimulia Bhinda na kuongeza:

“Nchunga alitakiwa kuachia madaraka ili aje mwenyekiti waliyekuwa wakimtaka wao, wakiamini wakiwa na kiongozi huyo, Yanga ingepata mafanikio makubwa… walifanya kila aina ya mbinu ili Nchunga aachie ngazi, lakini ilishindikana kutokana na mambo mbalimbali ya kikanuni.”

Bhinda anasema baada ya kuona wameshindwa, ikaja plani B ambayo ni Yanga kufungwa na Simba, tena kwa idadi kubwa ya mabao.

“Nakumbuka ilikuwa ni msimu wa mwaka 2011/12 wakati tulipofungwa hayo mabao matano na ndio mwisho kwa Simba kuchukua ubingwa wa Tanzania Bara.

“Kama unavyofahamu, mashabiki wa Simba na Yanga wakiamua jambo lao, huwezi kulizuia, baada ya kuona tumefunga yale mabao matano, Nchunga akalazimika kujiuzulu ili aje mwenyekiti ambaye walimtaka na hizi ndizo klabu za Simba na Yanga,” anasema Bhinda.

Anasema kuwa siku ile wachezaji wa Simba hawakuwa na uwezo wa kuifunga Yanga mabao 5-0, japo soka ni mchezo wa makosa.

“Kama unakumbuka, wachezaji wa Yanga walikuwa wakimuacha Emmanuel Okwi afanye anavyotaka, uongozi wa Simba chini ya Rage ukapata sifa ambazo hawakustahili, hawakujua inaingia kwenye rekodi, ona hadi hii leo tumeshindwa kuwafunga Simba yale mabao matano,” anasema Bhinda.

“Hadi hii leo sijui kama yale mabao matano yatatoka kwenye akili yangu. Wakati mipango ile inafanyika nilijua, lakini sikuwa na nguvu kwa vile nilikuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji, sikuwa na meno kama walivyokuwa wengine, lakini iliniuma kweli, kwani wakati naingia uwanjani, nilijua tunafungwa, lakini sikufahamu idadi ya mabao.”

Hata hivyo, Bhinda anatoboa kwa upande mwingine, inawezekana ushindi ule wa ‘dezo’ ndio ulioipa laana Simba na matokeo yake kushindwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara tangu msimu ule hadi sasa, ukiwa ni msimu wa nne sasa.

Anasema Simba wanatakiwa kulitafakari hilo kwa kina kabla ya kugeukia mambo mengine, wanapofikiria kurejesha zama zao walipokuwa wakipokezana na Yanga ubingwa wa Bara.

Japo Simba wamekuwa wakiuanza vema msimu, tangu wakati huo wamekuwa wakipotea maboya baada ya raundi kadhaa za msimu kama ilivyokuwa msimu uliopita, ambapo walianza vizuri na baadaye kuanza kuboronga.

Juu ya hali ilivyo ndani ya Yanga, Bhinda anasema kuna tofauti kubwa sana kati ya sasa na zamani, kwani awali kulikuwa hakuna matabaka kama ilivyo kwa sasa.

“Zamani Yanga ilikuwa na upendo, mchezaji akiwa na tatizo uongozi unalifahamu na kulitatua haraka, tofauti na sasa,” anasema.

Pia, anasema kitu kingine kinachomkera Yanga ya sasa ni kwamba mtu kama hana uwezo wa kifedha, hathaminiwi, watu wanashindwa kufahamu kuwa fedha si kila kitu katika maisha ya soka.

Alisema kuwa unaweza kuwa na fedha lakini usifahamu mpira, na baadhi ya watu wenye uwezo wa kifedha, hawajui mpira na wala hawazifahamu sheria 17 zilizowekwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -