Tuesday, December 1, 2020

BIFU KWENYE MUZIKI KITU CHA KAWAIDA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA ZAITUNI KIBWANA,

HIVI karibuni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, alitangaza kuwapatanisha wasanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba na Nasib Abdul ‘Diamond’, ili kufanya kazi kwa pamoja.

Kauli hiyo ya Mwakyembe imegeuka stori kubwa, hasa kwa wapenda burudani mbalimbali ambapo lengo kubwa la Waziri huyo ni kuwataka wasanii hao kumaliza bifu zao ili kufanya kazi kwa pamoja na kuendelea kukuza vipaji vyao.

Ujumbe huo umetafsiriwa kwa namna  tofauti, ambapo wapo waliompongeza Waziri huo kwa kuamua kuingilia bifu hilo, huku wengine wakimpinga vikali.

Wazo hilo siyo baya, lakini tukumbuke  kuwa moja ya mbinu zinazotumika na nyota mbalimbali duniani wa muziki ni ile ya kutengeneza bifu bandia na kuwahusisha mashabiki wao.

Mbinu hiyo inaonekana kusaidia kukuza idadi kubwa ya nakala za kazi za sanaa za wasanii hao wenye bifu ambapo wanaingiza fedha nyingi.

Kwenye hili nirejee bifu kati ya Juma Nature na Inspekta Haroun na ile ya wasanii wa East Coast Team na wale wa maeneo ya Temeke.

Japo haifahamiki vizuri historia ya bifu hizo mbili, lakini kwa hakika zilivuta hisia za wapenzi wengi wa bongofleva na kila mmoja alikuwa akiwafuatilia kwa karibu wasanii hao, japo kwa sasa makundi hayo yamevunjika.

Lakini pia nikumbushe lile bifu la Nasma Kidogo na Khadija Kopa jinsi walivyokuza muziki wa taarabu kwa kipindi hicho, ilikuwa kila unapokatisha lazima usikie majina ya wasanii hao, lakini baada ya Nasma kufariki muziki huo umepoteza mvuto, japo kuna waliojaribu kuurudisha bado hauwezi kuwa na dhamani ile kama kipindi kile.

Kwenye muziki wa dansi walikuwapo watu kama Banza Stone akiwa na TOT na Ally Choki akiwa na Twanga Pepeta. Unakumbuka walivyojenga majina makubwa kipindi hicho dansi ilikuwa dansi kweli, siyo sasa wamebaki wachache ambao pia hawana mvuto ule.

Hakuna asiyejua bifu linasaidia kazi za wasanii kupewa nafasi ya kujadiliwa kama wanavyojadiliwa wasanii waliopo kwenye bifu hizo.

Kikubwa bifu lengo lake ni kuwanufaisha kibiashara na mara nyingi zimekuwa zikiwatengenezea wasanii hela za maana na kuendelea kutamba.

Ndiyo maana leo hii unapotaja bongo fleva tu lazima utaje jina la Ali Kiba na Diamond, kwa sababu bifu lao limewafanya kujulikana zaidi, tofauti na hapo awali.

Ukweli usiopingika bifu zimewafanya wasanii hao kufanikiwa na ndiyo maana hakuna anayetaka bifu hilo limalizike, hata wenyewe sidhani kama wanataka hicho kitu kitokee.

Hivi kwa mfano hii leo, Ali Kiba na Diamond wanamaliza tofauti zao, wakapeana mikono na kufanya kazi pamoja, wewe shabiki utakuwa na hamu ya kuendelea kuwafuatilia?

Bifu ndiyo uhai wa biashara yao ya muziki. Wakija kupatana ndio itakuwa mwisho wa zama zao kama ilivyokuwa kwa marehemu Banza Stone na Ali Choki, ambaye kwa sasa bado yupo Twanga, ila amepoteza umaarufu ule wa miaka ya nyuma.

Mwenyewe Kiba na Diamond wanaomba usiku na mchana upinzani wao uendelee, ili waendelee kupiga fedha za maana, hivyo wakipatana hakuna atakayetaka kuwasikia.

Wazo la Mwakyembe siyo baya, ila huku kwetu bila bifu mambo yatakuwa hayaendi kabisa, angeliacha tu liendelee kwa manufaa ya wasanii hao.

Asikwambie mtu! Bila bifu kutakuwa hakuna Diamond wala Kiba na hizo ndizo zinawasaidia wasanii wengi kupiga hela kwa nyakati tofauti.

Leo hii Diamond na Kiba wamekuwa wakifanya vema hata nje ya Tanzania kwa sababu tu ya kuwa na mashabiki wengi waliokuwa wakiwafuatilia kwa karibu sana, hasa baada ya kuanzishwa kwa kazi zao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -