Wednesday, November 25, 2020

BLAGNON SASA PAMBANIA ‘FIRST ELEVEN’ YA OMOG

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA

SIMBA wamemrudisha mshambuliaji wao Fredrick Blagnon aliyekuwa kwa mkopo nchini Oman baada ya kushindwa kupatikana kwa wakati hati ya uhamisho (ITC).

Blagnon aliyezaliwa Desemba 26, mwaka 1985, alisajiliwa na Simba akitokea African Sport ya nchini kwao Ivory Coast, tayari ameungana na wenzake kwenye kambi ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Shrikisho (FA) na Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezaji huyo wa zamani wa Union Sportive de Bitam ya Gabon na Asante Kotoko ya Ghana, tangu alipojiunga na kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi kwa mkataba wa miaka miwili, alipachika mabao mawili pekee mzunguko wa kwanza.

Blagnon ambaye usajili wake ulizingatia zaidi umbile lake la urefu alishindwa kuendana na kasi na kuonyesha kiwango kilichotakiwa, licha ya kusajiliwa kwa gharama kubwa za Sh milioni 100.

Kuchemka kwake na kushindwa kuendana na kasi ya kocha Joseph Omog, kulisababisha kuondolewa kwenye kikosi cha kwanza kabla ya kuachwa jumla ndani ya kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi.

Baada ya kuachwa Simba ililazimika kusajili vifaa vingine ili kuweza kuboresha safu yao ya ushambuliaji, ambapo walisajiliwa wazawa Patrory Athanas na Juma Luizio ambao hata hivyo nao wameshindwa kuendana na kasi ya kikosi hicho na kulifanya jina la Blagnon kukumbukwa na mashabiki wengi.

Blagnon alikumbukwa kutokana na uhodari wake wa kupambana na mabeki ‘wabishi’ na kuwapiga vikumbo, huku akitoa mwanya kwa Ibrahim Ajib, Laudit Mavugo kufanya yao kirahisi.

Lakini sasa Blagnon amerejea na tayari yupo Arusha, hivyo kazi kwake kuhakikisha anapata namba kwenye kikosi cha kwanza ‘First Eleven’ cha Omog iliyobakisha michezo sita tu kabla ya kumaliza Ligi Kuu Bara.

Ikumbukwe awali Simba ilikuwa na tatizo kwenye safu yao ya ushambuliaji hasa katika eneo la umaliziaji, lakini kwa siku za karibuni mastraika wao wakiongozwa na mzawa Shiza Kichuya wamekuwa wakifanya vema.

Mastraika hao kwa siku za karibuni wamekuwa ndiyo roho ya Simba hasa baada ya kuhakikisha wanazifumania nyavu za wapinzani wao mara kwa mara na kuondoa tatizo sugu la safu hiyo ya ushambuliaji.

Ubora wa mastraika hao kwa sasa unaweza kusema si rahisi kuwaondoa kwenye kikosi cha Omog, hivyo Blagnon anapaswa kuonyesha kiwango cha hali ya juu ili kulishawishi benchi la ufundi.

Shiza, Mavugo na Ajib ndiyo waliowaondoa kwenye kikosi cha kwanza, Patrory Athanas na Juma Luizio kutokana na kuonyesha viwango hivyo kurudi kwa Blagnon anapaswa kuonyesha ubora wake.

Najua anatambua ushindani wa namba kwa sasa ndani ya kikosi hicho, ambapo jambo ambalo litamfanya awe salama ni kuhakikisha anaonyesha ubora mara dufu.

Kujituma, kupambana ndio silaha muhimu itakayokurudisha kwenye kikosi cha kwanza kwenye timu hiyo inayowania ubingwa baada ya kuusotea kwa miaka minne sasa.

Bila kujituma na kuonyesha kiwango utaendelea kusotea benchi kama afanyavyo kipa chipukizi Peter Manyika ambaye ameamua kugawa namba yake ya kudumu kwa mgeni Daniel Agyei.

Simba kuna wachezaji wengi ambao kila mmoja anahitaji kuonekana kwenye kikosi cha Omog, lakini kama hautajituma benchi lazima liwe makazi yako ya kudumu.

Hakuna asiyejua kama Simba safari hii imedhamiria ubingwa, hivyo sidhani kama watakuwa na masihara ya kuchagua wachezaji wa kikosi cha kwanza ambao hawajitumi.

Unapaswa kuonyesha kiwango ili uonekane kwenye kikosi cha kwanza cha  Omog, ambapo imesalia michezo sita ili kukamilisha duru hii ya pili ya Ligi Kuu Bara.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -