Wednesday, October 21, 2020

BOCCO AMPA KIBURI MBELGIJI

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA WINFRIDA MTOI

KOCHA mkuu wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba, Patrick Aussems, amefurahia kurudi uwanjani kwa nahodha wake, John Bocco, akiamini ataongeza nguvu katika mechi zijazo.

Bocco amemaliza kutumikia adhabu yake ya kukosa mechi baada ya kulimwa kadi nyekundu kutokana na kitendo cha kumpiga konzi mchezaji wa Mwadui FC, Revocatus Richard, katika mechi iliyochezwa Septemba 23 mwaka huu na kumalizika kwa Simba kushinda 3-1.

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), ilimfungia Bocco mechi tatu na kumlima faini ya shilingi laki tano.

Kutokana na adhabu hiyo, Bocco alikosa mchezo dhidi ya Yanga uliochezwa Septemba 30 na kumalizika kwa sare ya kutofungana, mechi na African Lyon waliyoshinda 2-1 na juzi dhidi ya Stand United walipoibuka kidedea na mabao 3-0.

Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Stand United, Aussems, alisema licha ya kumkosa nahodha wake katika michezo iliyopita bado waliendelea kufanya vizuri kwa sababu wana kikosi kipana.

Hata hivyo, kocha huyo raia wa Ubelgiji alisema Bocco ni mchezaji muhimu katika kikosi hicho ukizingatia wana michezo mitatu ndani ya siku nane na kusisitiza itakuwa ni faida katika kuongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji.

“Nawaamini wachezaji wangu wote wataendelea kufanya vizuri, ila natarajia mabadiliko zaidi baada ya kurudi kwa Bocco,” alisema Aussems.

Alisema katika mchezo wa juzi dhidi ya Stand United, aliwakosa wachezaji watatu lakini walioziba nafasi zao walicheza kwa kiwango kizuri bila kuwepo na pengo lolote.

Aussems alisema hali hiyo imechangiwa na kitendo cha kufanyia kazi mapungufu aliyoyaona kwa baadhi ya wachezaji, wakati ligi ilipokuwa imesimama kupisha michezo ya kufuzu Kombe la Afrika mwakani.

Mbelgiji huyo alisema katika mechi za nyuma walikuwa wanapata ushindi wa mabao machache, lakini kwa uwezo ulioonyeshwa juzi anaamini watabadilika zaidi na kupata mabao mengi.

“Kila mchezaji anaonekana kucheza kwa kujituma, mfano leo (juzi), nimewaanzisha Mohammed Ibrahim, Said Hamis ‘Ndemla’ na Jjuuko Murushid, wote wamefanya vizuri na tutaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Alliance ili kuendeleza wimbi la ushindi,” alisema Aussems.

Katika mchezo huo, Jjuuko alianza kutokana na Erasto Nyoni kusimamishwa na anapelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kumpiga kiwiko Hassan Nassoro Maulid wa Ndanda katika mchezo wao uliopigwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Ndemla na Mo Ibrahim walianza kutokana na kukosekana kwa James Kotei, ambaye na yeye suala lake la kumpiga ngumi Gadiel Michael wa Yanga likiwa katika kamati ya nidhamu huku Jonas Mkude akiwa majeruhi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -