Wednesday, September 30, 2020

Bocco: Hatutarudia makosa

Must Read

KISA KONA YA CARLINHOS… ...

NA ZAINAB IDDY BAO la Yanga lililofungwa na Lamine Moro juzi katika mchezo dhidi...

HUYU MUGALU ATAWALAZA WATU NA VIATU TU!

NA ONESMO KAPINGA HAKIKA sijapata utamu wa mshambuliaji mpya wa Simba, raia wa DR...

Wachezaji Gwambina wapewa muda

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa timu wa  Gwambina, Fulgence Novatus, amesema amewapa muda wachezaji wake ...

NA ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

BAADA ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting mwishoni mwa wiki iliyopita, benchi la ufundi pamoja na wachezaji wa timu hiyo, wameapa kutorudia makosa ya ‘kuchezewa sharubu zao’, hasa wanapoelekea kuvaana na Mwadui Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ni wa pili kwa Simba tangu ligi iliporejeshwa baada ya kusimamishwa tangu Machi 17, mwaka huu kutokana na hofu ya kuenea kwa maambukizi ya virus vya corona.

Wakiwa wanaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 72, Simba wanahitaji alama 14 ili kujihakikishia ubingwa wa ligi hiyo, ukiwa ni wa tatu mfululizo.

Pamoja na hilo, kitendo cha kutoka sare na Ruvu Shooting, kilionekana kutia doa malengo ya klabu hiyo kutangaza mapema zaidi ubingwa, huku wakiwa na michezo ya ‘kumwaga’ mkononi.

Ni kutokana na kufahamu hilo, benchi la ufundi na wachezaji wa Simba, wamewatioa hofu mashabiki na wanachama wao, wakiwaambia kuwa moto wao hautazimka kuanzia keshokutwa Jumamosi.

Akizungumza na BINGWA jana, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, alisema kuwa timu yake itaingia uwanjani kuikabili Mwadui ikiwa na nguvu zaidi ya ilivyokuwa dhidi ya Ruvu Shooting.

Sven alisema kuwa vijana wake wana kazi kubwa katika mechi inayokuja, kwasababu hawataangalia wala kudharau tena timu watakayokutana nayo kwani wanatafuta ushindi kwa namna yoyote.

“Kwa namna ligi inavyoendelea, kuna ushindani sana na Simba inahitaji kuwa bingwa, tuliwadharau Ruvu tukapata sare, hatutafanya tena makosa hayo, kila tutakayekutana naye, tutaupa uzito mchezo, tutauchukulia kama ndio utakaotupa ubingwa.

“Makosa tuliyoyafanya katika mechi na Ruvu yalikuwa yanaweza kuepukika, baada ya mechi tumekaa na kujadili kwa pamoja na kukubaliana kuanzia mechi na Mwadui, hatuhitaji sare wala kupoteza zaidi ya pointi tatu,” alisema.

Kwa upande wake, Bocco alisema: “Tunafahamu kuwa mashabiki wetu wana shauku kuona tunatangaza mapema ubingwa na hawapo tayari kuona tunafungwa au kupata sare.

“Tumekaa na benchi la ufundi na kukubaliana kwamba katika mchezo wote ujao na Mwadui, tunakuwa makini zaidi ili tupate pointi zote tatu. Itakuwa hivyo kwa kila mchezo uliopo mbele yetu hadi pale tutakapotangaza ubingwa, hivyo mashabiki wetu wasiwe na wasiwasi na badala yake, waendelee kutupa sapoti.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

KISA KONA YA CARLINHOS… ...

NA ZAINAB IDDY BAO la Yanga lililofungwa na Lamine Moro juzi katika mchezo dhidi...

HUYU MUGALU ATAWALAZA WATU NA VIATU TU!

NA ONESMO KAPINGA HAKIKA sijapata utamu wa mshambuliaji mpya wa Simba, raia wa DR Congo, Chris Mugalu,kutokana na jinsi...

Wachezaji Gwambina wapewa muda

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa timu wa  Gwambina, Fulgence Novatus, amesema amewapa muda wachezaji wake  ili aweze kutathimini kiwango cha...

Kisu amfunika vibaya Manula

NA ZAINAB IDDY KIPA  wa timu ya Azam, David Kisu, amemfunika Aishi Manula  wa Simba kutokana na kutoruhusu...

Zahera awapa Simba taji mapema

NA ZAINAB IDDY BAADA ya Gwambina kufungwa mabao 3-0 na Simba  katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -