Wednesday, October 28, 2020

BOCCO, KAPOMBE KUWAKOSA MTIBWA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MASYENENE DAMIAN, MWANZA

NAHODHA wa Simba, John Bocco na beki wa kulia wa timu hiyo, Shomari Kapombe, wanatarajiwa kuukosa mchezo wa leo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, jijini hapa dhidi ya Mtibwa Sugar kwa kuwa ni majeruhi.

Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi hao, kilitua jana saa tatu asubuhi kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza na kupokewa na mamia ya mashabiki wa timu hiyo, tayari kwa mchezo huo.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, waliwasili jijini hapa wakitokea Arusha walikocheza dhidi ya Arusha United na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, yakipachikwa na Emmanuel Okwi.

Baada ya kupokewa na mashabiki, kikosi cha Simba kilielekea katika Hoteli ya Renana iliyopo Pasiansi, wilayani Ilemela kupumzika kujiweka sawa kwa mchezo huo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, alisema kikosi chake kimekamilika isipokuwa wachezaji hao wawili ambao bado hawajawa na uhakika wa kuwatumia kwa mchezo wa leo.

“Tumefanya maandalizi ya mwezi mmoja, kikosi chetu kiko sawa hatujapoteza mchezo wa maandalizi, nyota wote wa Simba watakuwepo isipokuwa Kapombe na Bocco ambao bado wanaendelea na matibabu, kuwatumia kesho (leo) tutakuwa tumeharakisha sana.

“Nadhani watakuwa tayari Jumatano ligi itakapoanza, ligi inaanza Jumatano kila mtu yuko tayari, wengine hawana matatizo….mbinu zetu wapinzani watazijua kesho (leo) na kila kitu tunaendelea kukipanga na wachezaji namna ya kuucheza mchezo wa kesho (leo),” alisema.

Katika mchezo huo wa Ngao ya Jamii, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, akisindikizwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Maria, ambapo viingilio kwa jukwaa kuu (VIP) ni Sh 10,000, mzunguko (kawaida) ni Sh 5,000 na Sh 1,000 kwa wanafunzi.

Mchezo huo pia ulitanguliwa na kongamano la michezo lililoandaliwa na TFF (TFF Football Summit) likishirikisha wenyeviti wa vyama vya michezo vya mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na Rais wa TFF ambalo lilifanyika jana kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -