Saturday, November 28, 2020

BOCCO KUONGOZA ‘MAUAJI’ YA MBABANE SWALLOWS

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA SAADA SALIM

MATUMAINI ya Azam FC kuibuka na ushindi dhidi ya Mbabane Swallows katika mchezo wa marudiano wa michuano ya Kombe la Shirikisho yamebebwa na mshambuliaji wa timu hiyo, John Bocco.

Bocco ni miongoni mwa wachezaji wa Azam walioondoka jijini Dar es Salaam juzi  kuelekea Afrika Kusini, kisha Swaziland kwa ajili ya kuikabili Mbabane Swallows ya nchini humo katika pambano la pili la michuano ya Kombe la Afrika.

Azam, ambayo imepiga kambi ya muda mfupi katika jiji la Pretoria, Afrika Kusini,  leo itaondoka nchini humo kuelekea Swaziland tayari kwa mchezo huo, utakaopigwa kesho Jumapili jijini Mbabane.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Azam ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mshambuliaji John Bocco hakuwa sehemu ya kikosi cha Azam kilichoibuka na ushindi kwenye mchezo huo, kutokana na kuwa  majeruhi, baada ya kuumia wakati wa mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Kurejea kwa mshambuliaji huyo na kusafiri na timu hiyo kumerejesha matumaini makubwa kwa mashabiki wake, kwani ataimarisha safu hiyo ya ushambuliaji, huku akisaidiana na Yahaya Mohammed ambaye alisimama mbele akisaidiana na Ramadhani Singano.

Meneja wa timu hiyo, Philip Alando, ameliambia BINGWA jijini jana kuwa, wachezaji wao, Bocco, Himid Mao na Stephan Kingue wako fiti kuikabili Mbabane.

“Wachezaji wana shauku kubwa, kazi iliyobaki ya kocha kuwafundisha mbinu za kusaka ushindi, tuna imani kubwa tutapata matokeo mazuri katika mchezo wa marudiano na kusonga mbele hatua inayofuata,” alisema Alando, ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Kagera Sugar.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -