Saturday, October 31, 2020

BOCCO: MTIBWA  WAMETUTOA TONGOTONGO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWAMVITA MTANDA

NAHODHA wa timu ya Simba, John Bocco ‘Adebayor’, amesema kwamba mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sufar  imewatoa tongotongo na kuwafungulia milango ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayoanza kutimua vumbi kesho.

Jumamosi iliyopita Simba walinyakua kombe la Ngao ya Jamii baada ya kuwatandika Mtibwa mabao 2-1, katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kurumba, Mwanza.

Akizungumza na BINGWA jana, Bocco alisema kwa sasa   Simba wanahitaji kutetea ubingwa wa Ligi Kuu na si vinginevyo, hivyo fursa waliyoipata ya kuwafunga Mtibwa imewafungulia njia ya kufanya vizuri katika ligi hiyo itakayoanza kesho.

“Si unajua nyota njema huonekana asubuhi, tumecheza mechi kadhaa za kirafiki lakini tulikuwa tunatoka sare na kule mkoani Arusha tulishinda 2-1 dhidi ya Arusha United.

“Mchezo wa Ngao ya Jamii umetufungulia milango ya kupambana katika Ligi Kuu maana tumeanza vizuri, sasa ni kama tumejihakikishia kuwa hata mwaka huu ubingwa utakuwa wa kwetu,” alieleza Bocco.

Aidha, Bocco alisisitiza kwamba kikosi cha Simba cha msimu ujao kimejipanga zaidi ya msimu uliopita, hivyo maajabu yataendelea kuonekana kutokana na timu yao ilivyo imara.

“Kawaida timu inapopata ushindi faida haitakuwa kwa klabu pekee bali ni kwa mashabiki na wanachama kwa ujumla, sisi tunawaahidi kwamba tutaendelea kunapambana kwa ajili yao,” aliongeza Bocco.

Wekundu hao wa Msimbazi wamepangwa kufungua pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu kwa kumenyana na Tanzania Prisons kesho katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -