Saturday, November 28, 2020

Bokungu afuta jina la Kessy Msimbazi

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA

BEKI Janvier Bokungu, anayecheza namba mbili katika kikosi cha Simba, amefuta rasmi jina la Hassan Ramadhani ‘Kessy’ kwenye vichwa vya mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi hao.

Kessy alikuwa ni mchezaji tegemeo mno katika kikosi cha Simba, akionekana kuziba vilivyo pengo la watangulizi wake kama Shomari Kapombe, Miraji Adam na Nassoro Chollo.

Baada ya Kessy kutimkia Yanga, akifanya hivyo kwa nyodo, mashabiki wa Simba walionekana kuweweseka kwa hofu ya kukosa mbadala wake.

Hivyo, Wekundu wa Msimbazi hao walianza kutangaza kupinga usajili wa beki huyo wa kulia katika kikosi cha watani wao hao wa jadi, kwani alielezwa kusaini mkataba wakati akiwa bado ni mali yao.

Hapo ndipo matukio kadha wa kadha juu ya sakata la mchezaji huyo yalipofuata, ikiwamo kumkatia rufaa kwa Kamati ya Usajili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Katika hilo la usajili, Wekundu wa Msimbazi hao ‘waliangukia pua’, wakiambiwa kuwa mashtaka yao ni ya kimadai zaidi na hayawezi kumzuia Kessy kusajiliwa na timu yoyote.

Wakati sakata la Kessy likiendelea, Simba ilikuwa ikifanya usajili na kufanikiwa kunasa wachezaji kadhaa wa kuziba pengo la beki huyo wa kulia, wakiwamo Bokungu na Malika Ndeule na Hamad Juma.

Kati yao, Bokungu ameonekana kukata kiu ya wapenzi wa Simba ambao pole pole wameanza kumsahahu kabisa Kessy na kwamba dalili zinaonyesha kutokuwa na muda wa kuendelea kufuatilia sakata lake.

Hilo linatokana na ukweli kwamba, Mkongomani ameonyesha kiwango kizuri kwenye michezo mbalimbali ya Simba iliyopita, ukiwamo ule dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga.

Bokungu mbali na uwezo wa hali ya juu aliouonyesha katika kukaba, ni mrefu kiasi cha kumwezesha kucheza mipira ya juu kwa ufanisi mkubwa kama ilivyo katika kupandisha timu pale ilipohitajika.

Zaidi ya hayo, Bokungu ameonekana kuwa makini mno anapokabiliana na washambuliaji wa timu pinzani, ikiwamo kusaidia ulinzi wa kati pale mabeki wa kati walipopanda kusaidia mashambulizi au vinginevyo.

Na sasa beki huyo tayari ameingia katika vichwa vya wapenzi wa Simba, akichukuliwa kama mmoja wa wachezaji muhimu ndani ya kikosi cha Wekundu hao, akiwa amewapiga kumbo wenzake wanaogombania nafasi hiyo, Ndeule na Juma ambao wote wamejikuta wakikosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Kocha Mkuu, Joseph Omog.

Akizungumza na BINGWA jana, shabiki wa Simba kutoka tawi la Buguruni, Dar es Salaam, Maria Israel, alisema Bokungu amedhihirisha ubora wake hasa kwenye mechi ya Yanga alipoweza kuwadhibiti washambuliaji machachari wa Yanga hasa Donald Ngoma.

“Wote mtakubaliana na mimi kwamba Bokungu ‘alimtia mfukoni’ Ngoma wa Yanga tofauti na ilivyokuwa kwa Kessy ambaye alikuwa akirukaruka tu uwanjani tunapocheza na Yanga,” alisema.

Safu ya ulinzi ya kikosi cha kwanza cha Simba mbali ya Bokungu, inaundwa na wachezaji makini mno ambao ni Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ anayecheza namba tatu, Novaty Lufunga, Method Mwanjali na Jjuuko Murushid ambao hupewa ulinzi mkali na kiungo mkabaji mzoefu ambaye ni nahodha wa Wekundu wa Msimbazi hao, Jonas Mkude.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -