Saturday, November 28, 2020

BONDIA MATUMLA ATOKA MOI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA VERONICA ROMWALD

BONDIA Mohamed Matumla (30) aliyekuwa amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI), ameruhusiwa kurudi nyumbani.

Akizungumza na BINGWA, Ofisa Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi, alisema Matumla aliruhusiwa jana na madaktari wake ambao walijiridhisha maendeleo ya afya yake kuwa ni mazuri.

“Tunapenda kuwaarifu wanamichezo wote hususani wapenzi wa mchezo wa ngumi Tanzania kwamba tumemruhusu Matumla kwenda nyumbani. Tumejiridhisha kwamba afya yake imetengamaa vizuri,” alisema.

Mvungi alisema wataendelea kumfuatilia kama mgonjwa wa nje kwenye kliniki zao.

“Hivyo tuendelee kumwombea ili afya yake iendelee kuimarika zaidi.”

Bondia huyo hivi karibuni alifanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo kuondoa damu iliyokuwa imevilia ndani ya kichwa chake.

Alipatwa na hali hiyo, baada ya kupigwa ngumi kichwani na bondia mwenzake, Mfaume Mfaume katika raundi ya saba katika pambano lisilo la ubingwa lililofanyika hivi karibuni, jijni Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa MOI, Dk. Othuman Kiloloma, alisema Matumla atalazimika kukaa nje ya ulingo kwa kipindi cha miezi minane hadi 12 baada ya kufanyiwa matibabu.

Alisema atarejea ulingoni baada ya kuisha kwa muda huo hata hivyo atalazimika pia kupata kibali cha daktari.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -