Tuesday, October 20, 2020

Bonucci aliitosa Chelsea, City kumuuguza mwanawe

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

TURIN, Italia

BEKI wa Juventus, Leonardo Bonucci, alizitosa klabu za Ligi Kuu England dirisha la usajili la majira ya kiangazi kutokana na mwanawe wa kiume kuwa na hali mbaya kiafya, vimesema vyombo vya habari vya Italia.

Nyota huyo wa Juventus alikuwa akihusishwa na klabu za England, ambazo ni Chelsea, Manchester City na Manchester United.

Usajili wa Bonucci ulishindikana na kubakia kwenye klabu huyo ya mjini Turin na jarida la AS la Hispania kuweka wazi kwamba kilichosababisha kushindikana kwa usajili huo ni mtoto wa beki huyo, Matteo.

Mtoto huyo wa miaka miwili amekuwa akisumbuliwa na matatizo mbalimbali ya afya na miezi ya hivi karibuni alifanyiwa upasuaji.

Uhamisho huo ungemwongezea matatizo mtoto wake na taarifa zinasema kwamba ndio maana Bonucci hakutaka kuondoka Juve.

Lakini taarifa zinadia kwamba, Chelsea bado wanamfukuzia Bonucci kwa ajili ya kujaribu tena kumnasa usajili wa dirisha dogo la Januari mwakani, baada ya kuwa na mwanzo mbaya msimu huu.

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte, aliyekuwa akiinoa Juventus anataka kuungana na beki wake huyo wa zamani, baada ya kushuhudia kikosi chake kikichapwa na Liverpool na Arsenal, huku beki wake, Gary Cahill, akionekana kushindwa kumudu kucheza katika mfumo wake.

Kocha huyo wa Italia, alikuwa tayari kutumia pauni milioni 60 kwa ajili ya kunasa saini ya Bonucci.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -