Saturday, November 28, 2020

BOSSOU ANUNUA KESI YA AJIB

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR

BEKI wa kimataifa wa Yanga, Vicent Bossou, amewaangalia kwa jicho la tatu washambuliaji wa Simba, Ibrahimu Ajib na Laudit Mavugo, akisema anawasubiri kwa hamu Februari 25, mwaka huu, akisisitiza watajuta kumfahamu.

Bossou ambaye alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Togo kilichoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika mwaka huu (Afcon 2017) zilizomalizika mwezi uliopita nchini Gabon, ameonekana kulipania vilivyo pambano hilo la watani wa jadi litakalopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Kwa kufahamu kuwa Mavugo na Ajib ndio washambuliaji pekee katika safu ya ushambuliaji ya Simba wanaoweza kuwapa wakati mgumu, Bossou ameamua kuongeza mazoezi ya ziada ya viungo kuwakabili washambuliaji hao.

“Nakwenda ‘gym’ (klabu ya mazoezi ya viungo) kila asubuhi. Lakini nikwambie kitu? Najiandaa kufanya kitu fulani adimu (surprise). Sikwambii ni kitu gani. Mashabiki waje uwanjani kujionea,” alitamba Bossou.

Japo watu wa Simba wamekuwa wakiwatambia Ajib na Mavugo kuelekea mchezo huo, Bossou alijibu kwa dharau: “Si walicheza wote mechi iliyopita? Walifanya nini? Tena wakati wanatoka niliwasindikiza. Nimerudi kivingine, wenyewe wanajua nilikuwa wapi. Subirini hiyo siku ya mechi mtaona.”

Oktoba mosi, mwaka jana, timu hizo zilipokutana Uwanja wa Taifa, kamera za waandishi wa habari zilimnasa Bossou akimkejeli Mavugo wakati akitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Fredrick Blagnon kutokana na kushindwa kufurukuta kwa jinsi alivyomdhibiti.

Ajib na Mavugo wameonekana kuwa katika kiwango cha juu kwa siku za hivi karibuni, wakiunda muunganiko wa aina yake ulioisaidia Simba kushinda mechi zao kadhaa za ligi, ukiwamo ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Prisons mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -