Sunday, October 25, 2020

BOSSOU ATAKA YANGA WASAHAU SHIDA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA HUSSEIN OMAR


BEKI wa zamani wa Yanga, Vincent Bossou, amewataka wachezaji wa timu hiyo kusahau matatizo na shida zinazowakabili na kucheza mpira kwa juhudi mafanikio watayaona baadaye.

Bossou raia wa Togo, alikuwa tayari kurejea Jangwani hata bure ili kukitumikia kikosi hicho, baada ya awali kuachana nao kwa kutofautiana katika dau la kuongeza mkataba.

Lakini baada ya kubaini kikosi chake hicho kinakabiliwa na ukata, amewataka wachezaji wa timu hiyo kucheza kwa ari ili kuikomboa timu hiyo.

Akizungumza na BINGWA kwa mtandao kutoka kwao Togo, Bossou alisema taarifa zote za Yanga anazo na anajua fika kwamba timu hiyo kwa sasa hivi haina mfadhili na kuwataka wachezaji wa timu hiyo kupambana.

“Wapambane tu, timu haina mfadhili ndio lakini ipo siku atakuja mtu mwenye uwezo wa fedha na kuiongoza Yanga, matatizo mengi lakini Mungu yupo,” alisema.

Bossou alieleza tatizo kubwa linaloikabili Yanga hivi sasa ni ujuaji wa   viongozi, kwani kila mtu anajifanya bosi wakati hana mchango katika timu hiyo.

Alisema anawatakia kila la kheri mabingwa hao wa zamani Ligi Kuu Bara, katika harakati zao za kusaka ubingwa msimu huu na kuipeperusha vyema Bendera ya Tanzania katika michuano ya kimataifa.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -