Wednesday, November 25, 2020

Bossou awakejeli Mavugo, Ajib

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR,

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, beki wa Yanga, Vicent Bossou, alionekana kuwakejeli washambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo na Ibrahim Ajib, wakati walipokuwa wakifanyiwa mabadiliko.

Beki huyo wa Kimataifa wa Togo, alianza kumkejeli Mavugo wakati akitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Fredrick Blagnon, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa mwishoni mwa wiki Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Bossou alionyesha ishara kwamba Mavugo kachemsha ndiyo maana anatolewa, ambapo alizungusha mikono yake miwili wakati Mavugo alipokuwa akienda nje, hali ambayo iliibua hisia mbalimbali kutoka kwa mashabiki wa timu hizo mbili kongwe hapa nchini.

Beki huyo alionekana kumsindikiza Mavugo hadi nje ya uwanja, huku akimsemesha maneno na kumuonyesha ishara ya mabadiliko.

Katika mchezo huo wa juzi ambao uliishia kwa sare ya bao 1-1, Bossou alionekana kuwadhibiti vyema washambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo na Ibrahim Ajib.

Bossou alifanya kitendo kama hicho tena wakati Ajib akitoka, huku akionyesha zaidi ishara ya kuwaweka mifukoni washambuliaji hao ambao katika mechi hiyo hawakuwa na makali.

Ajib na Mavugo walishindwa kufurukuta mbele ya Bossou na kuifanya safu ya ulinzi ya Yanga kutamba muda wote wa mchezo huo, kabla ya Simba kusawazisha bao dakika ya 87 kupitia kwa Shiza Kichuya, aliyepiga kona iliyoingia moja kwa moja.

Timu hizo ambazo zimekuwa zikitambiana kwa muda mrefu, kila moja ikisema itamtoa mwenzake nishai, zilijikuta zikitoka sare ambapo bao la Yanga lilifungwa na Amis Tambwe, huku lile la Simba likifungwa na Kichuya.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -