Saturday, October 31, 2020

BOSSOU AWAPA YANGA VIFAA VIWILI HATARI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

SALMA MPELI NA HUSSEIN OMARY                  |               


 

BEKI wa zamani wa Yanga, Vincent Bossou, amewapa Yanga wachezaji wawili wa kimataifa wa Nigeria, kwa ajili ya kuboresha kikosi chao litakapofunguliwa dirisha dogo la usajili Desemba, mwaka huu.

Akizungumza na BINGWA jana, Bossou ambaye kwa sasa anakipiga katika kikosi cha Binh Duong FC ya Ligi Kuu nchini kwao Togo, aliwataja wachezaji hao kuwa ni Ezika Caleb Kelechi anayecheza nafasi ya winga na Moneke Ugochuku Obi ambaye ni mshambuliaji.

Alisema wachezaji hao wote ambao wanacheza timu ya Taifa ya vijana ya Nigeria, kwa sasa wapo huru na kwamba ameona wanaweza kuisaidia Yanga iwapo wataongezwa kwenye kikosi chao.

“Hawa ni wachezaji wazuri na vijana ambao wanaweza kuisaidia Yanga kwa sasa katika nafasi hizo mbili kutokana na mapungufu ya kikosi chao,” alisema Bossou.

Bossou ambaye aliitumikia Yanga kwa misimu miwili tofauti, aliachana na klabu hiyo Mei mwaka jana baada ya mkataba wake kumalizika na kushindwa kuendelea na Wanajangwani hao.

Yanga ambayo kwa sasa inaonekana kuwa na mapungufu kwenye kikosi chao, licha ya kumsajili straika kutoka DR Congo, Heritier Makambo, bado wanaonekana kuhitaji kukiongezea nguvu zaidi kikosi chao kuhimili mikikimikiki ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -