Thursday, October 29, 2020

BRADLEY LOWERY ALIVYOISHUHUDIA SUNDERLAND KWA MARA YA MWISHO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

London, England

SHABIKI mkubwa wa Sunderland, Bradley Lowery, alishangiliwa na mashabiki wengine wa klabu hiyo kwenye Uwanja wa Light na kupata nafasi ya kufunga goli dhidi ya mlinda mlango wa Chelsea, Asmir Begovic.

Mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitano, anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani na alikuwepo uwanjani kabla ya mchezo wa Ligi Kuu England kati ya klabu yake ya Black Cats dhidi ya Chelsea.

Kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa huo wa saratani kwa mara ya pili, Bradley, inadaiwa kwamba shabiki huyo hataweza tena kukutana na watu kama hivyo wiki kadhaa zijazo, ili kusaidia kinga ya mwili wake, kutokana na kudaiwa kubakiza miezi miwili ya kuishi.

Hivyo mtoto huyo alitumia muda wake kwenye uwanja wa klabu yake anayoipenda, akikumbatiana na kinara wa mabao wa Sunderland, Jermain Defoe, kabla ya mpira kuanza.

Pia alitumia muda wake na mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa, akipiga picha na karibia kikosi kizima cha Blues kilichoanza kwenye mchezo huo wa juzi Jumatano.

Sunderland walionyesha heshima kwa shabiki wao huyo, baada ya kubandika jezi ya mtoto huyo ikiwa na jina na namba tano mgongoni mwake.

Bradley alipata fursa ya kutembelea uwanja wa mazoezi wa Sunderland, ambapo kocha wa Black Cats, David Moyes, alisema: “Bradley alikuja tangu mchana na kumtembeza kwenye ‘gym’ na kwenye bwawa la kuogelea.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -