Sunday, November 29, 2020

BRAVO PLUIJM KWA KUISUKA YANGA IMARA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Na Kelvin Lyamuya

MCHAKAMCHAKA wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara msimu huu unazidi kunoga.

Wale walioanza kwa vicheko walicheka haswa, lakini kwa sasa upepo wa furaha umewageukia wale walioanza kwa kuchechemea, mwanzo wao uliokuwa mgumu unaelekea kumalizika kwa raha.

Mabingwa watetezi Yanga ambao wana jukumu la kuhakikisha wanatetea ubingwa wao pamoja na kuilinda heshima kubwa waliyoipata msimu ujao, wamebakisha takribani mechi 10 za kumaliza mtihani mgumu waliouanza.

Mwanzoni mwa safari yao ya kulitetea taji hakuna aliyediriki kufungua kinywa chake na kusema kwamba Yanga itasalia kwenye ubora wao.

Wengi walitishwa na hali ya uchovu ambayo kimsingi ilisababishwa na kushiriki michuano mingine tofauti na ligi kuu.

Kwa msimu huu wa 2016/17, Yanga haikuwa na cha kutarajia zaidi ya changamoto kutoka kwa timu za ligi kuu, kilichowafanya wadau wasiwe na imani juu yao ni kwamba kila timu ilijiandaa; African Lyon yenye morali, Mwadui na Kagera zisizo na woga kwa yeyote, Mtibwa yenye soka maridhawa na Simba iliyoamka.

Lakini mimi binafsi niliamua kuwa wa mwisho kuamini kama Yanga yenye rekodi murua ya kubeba mataji 26 ya ligi, kuwa ingetoka kwenye tatu bora ya msimamo wa ligi msimu huu.

Sababu zilikuwapo na niliamini wangecheza kwa nguvu kubwa zaidi ya ile ya msimu uliopita. Hakuna kinachoshindikana chini ya jua.

Mkurugenzi wa ufundi ambaye alihamishwa kitengo kutoka kuwa kocha mkuu, Hans van Pluijm, aliitengeneza Yanga ya ushindi ambapo hakuna aliyefikiria kuwa ina uwezo wa kucheza soka la nguvu na kasi kwa miaka mingine mitano ijayo.

Hawa wachezaji mnaowaona hivi sasa; Simon Msuva, Thaaban Kamusoko, Haruna Niyonzima na wengineo walifundishwa moja ya kitu muhimu kwenye soka ambacho ni nidhamu ya kusaka ushindi.

Kabla ya Pluijm kubadilishiwa majukumu, niliamini asingepata shida tena msimu huu kwa sababu alijiandaa kwa miaka mingine mitano mbele.

Kitendo cha kuwaunganisha hawa wachezaji, wakawa na umoja na kuja kwa George Lwandamina pamoja na nyongeza ya wachezaji, ni jambo la faida linalowafanya Yanga kutoonekana kama ndio wale waliotabiriwa kutetereka kwa uchovu.

Niliamini mabadiliko machache waliyoyafanya hasa kwa kuyaongezea nguvu maeneo muhimu, ungewawezesha kusalia kwenye ubora wao msimu huu.

Nakumbuka Pluijm alirejea Yanga 2014 ili kuliokoa jahazi la Yanga lililokuwa ‘linazamishwa’ na Marcio Maximo, ametimiza miaka mitatu ya kuwapo Jangwani na jukumu kubwa alilopewa ni kurudisha nidhamu ya kikosi, jambo alilolitimiza hadi kufikia hivi sasa mnapoiona Yanga ya mwendokasi.

Kabla ya ujio wa Lwandamina, Yanga ilikuwa kwenye mikono salama ya Pluijm ambaye alidhihirisha uwezo wake wa kuhimili mfululizo wa presha katika kila msimu.

Ninachoamini, Yanga hii ninayoishuhudia tena msimu huu ni ile ile ya Pluijm.

Lwandamina amekuja katika kipindi kizuri ambacho ana uwezo wa kuitengeneza himaya yake, lakini kasi, nguvu, mabao makali, pumzi ya kutosha ilitengenezwa na Pluijm.

Mbinu bora za ushindi zilipandwa na Plujim na mbinu hizo zimekuza kiwango bora kabisa cha Yanga kinachopasua ardhi na kupanda hadi juu, kileleni mwa msimamo wa ligi kuu.

Yanga inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi moja baina yao na Simba (mchezo wa kwanza zilitoka sare ya 1-1). Imeiacha Azam kwa tofauti ya pointi tisa (mchezo wa kwanza ulimalizika kwa suluhu).

Ni wazi hizi timu mbili pia zinautaka ubingwa msimu huu ili kutimiza ndoto zao ni lazima zifanye kitu mzunguko huu wa pili (kumfunga Yanga).

Ndio, wafanye hivyo ili tusimtangaze bingwa mapema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -