Friday, December 4, 2020

BURIANI ISMAIL MRISHO KHALFAN, DUNIA YA SOKA LA TANZANIA HAITOKUSAHAHU

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA HASSAN BUMBULI

WAKATI namalizia shughuli zangu jioni ya Jumapili, mara anakuja mmoja wa makamanda  wangu katika kazi na kuniambia juu ya mchezaji aliyeangua uwanjani kuwa amefariki.  Tuliangalia pamoja mechi ile japo  mimi sikuwa na muda wa kuitazama yote.

Tulio la kufunga  kwa mchezaji huyo nililishuhudia, na makandokando yote yaliyotokea kujaribu kumnusuru niliyaona, hadi pale alipopandishwa kwenye gari la Zima Moto kupelekwa hospitali niliona na kisha baadaye nikatoka na kuendelea na kazi ngine.

Kuna mamabo tulianza kujadili hata kabla yzaji huyo, mambo mengi yalijitokeza  baada ya mchezaji huyo kuanguka na kushindwa kuinuka. Nani alipaswa kufanya nini pale uwanjani?  Na nani alipaswa kuwajibika katika suala gani kwenye tukio lile? Haya na mengine mengi ni maswali ambayo mtu anapswa kujiuliza.

Taarifa za kifo cha mchezaji huyo chipukizi Ismail Mrisho Khalfan wa Mbao FC, zilishtua sana hasa kutokana na mazingira ya kuanguka kwake ikielezwa kwamba amechezewa rafu na mchezaji wa timu ya vijana ya Mwadui.

Kwa ambao walisikia tu kwamba mchezaji kachezewa rafu wengi walilalama na kulaumu rafu za hovyo za wachezaji wetu wa kibongo, wengine walianza kuwataja wachezaji wenye rafu za hovyo kwenye Ligi Kuu, na wengine walikwenda mbali na kuikumbuka rafu aliyochezewa Mnigeria, Abasirim   Chidiebere anayekipiga Stand United wakati walicheza na Azam FC.

Hawa ni wale ambao hawakuona tukio, kwa tulioliona tulizo la Ismail hali ilikuwa tofauti kabisa kwani, chipukizi huyo hakuchezewa rafu, kilichofanyika  katika mpira kinaitwa ‘Tackling’ beki Yule aliingia kuucheza mpira na hakumgusa kabisa mchezaji kwa maana na kumdhuru. Hakuwa na dhamira ya kumdhuru ndiyo maana alilala chini akacheza mpira na katika mazingira yake mambo mawili hutokea, ama mchezaji mwenye mpira aanguke  au amruke beki alitelala chini.

Kwa bahati mbaya, Ismail alinguka sambamba na beki, na wote walikuwa katika harakati za kuinuka kuendelea na mchezo, beki wa mwadui aliinuka na Ismail alijaribu kuinuka lakini akashindwa. Na ndiyo ulikuwa mwanzo wa mengi kutokea wakati akipatiwa huduma ya kwanza uwanjani, na kwa bahati mbaya huduma ya kwanza ilitolewa na watu ambao hawakuwa na ujuzi huo.

Baada ya huduma kwa kwanza kuonekana haifai kitu, Ismail alitakiwa kupelekwa hospitali, na sote tulishuhudia miondombinu iliyotumika kumpeleka kijana huyo hospitalini.  Pumzika kwa amani Ismail, dunia ya wanasoka itaendelea kukumbuka, huduma yako ndani ya dimba ilikuwa bado inahitajika sana kwa taifa hili la Tanzania na hakika tumekupoteza wakati tukiwa bado hatujafaidi matunda ya kipaji chako cha hali ya juu.

Pamoja na mazingira yote, pamoja na kwamba kiimani tunaamini kwamba mwenyezi Mungu ndivyo alipanga itokee, lakini kuna masuala ya msingi ambayo tunaweza kuyajadili na hayapaswi kupita hivihivi . mfano suala la kutokuwepo na gari la kubeba wagonjwa lilalotambuka pale uwanjani  ni moja ya mambo ambayo Shirikisho la Soka Tanzania wenye michuano hiyo wanapaswa kulitolea majibu ya kina sana.

Tumeshuhudia mchezaji yule akipandishwa kwenye gari za Zimamoto, gari ambalo halina huduma yoyote ya kwanza kwa mgonjwa na kimsingi halipaswi kubeba mfunjwa. Najiuliza Zimamoto ilifuata nini uwanjani pale?  Ilikuwaje zimamoto ikawa muhimu kuwepo uwanjani kuliko  gari la wagonjwa?

Michuano yah ii ya vijana inaratibuwa na TFF, na inafanyika katika vituo viwili, ni ajabu kuona michuano kama hii ya kitaifa inaendeshwa kama mashindano ya kugombea Mbuzi kwa kukosekana kwa huduma muhimu kama gari la wagonjwa.

Tukio hili ni sehemu tu matukio mengi yanayotokea kwenye viwanja ya mikoani hasa kwenye mechi za madaraja ya chini kama vile Lidi daraja la Kwanza, la Pili na kama hii ambayo inaendelea. TFF wamekuwa makini kwa kiasi fulani kwenye mechi za Ligi Kuu pekee ambazo hata hivyo kwenye maadhi ya viwanja kumeripotiwa mara kadhaa kutokuwepo kwa madagari ya kubeba waginjwa na wakati mwingine kukosekana huduma muhimu za usalamawa afya ya wachezaji na mashabiki viwanjani.

Kwa hali ilivyo nadiriki kusema hali ya usalama wa afya wa wachezaji na mashabiki viwanjani ni tete kwa Tanzania. Mungu atuepushe mbali na matatizo kama haya ambayo yamejitokeza lakini ukweli TFF inapaswa kusimamia  suala la usalama wa afya ya wachezaji kwa kuhakikisha wanakuwepo huduma zote muhimu za kwanza zinakuwepo .

Inasikitisha kuona uwanja kama wa Kaitaba upo katika Makao Makuu ya Mkoa unakosa huduma ya gari la wagonjwa wakati,  si mbali na sifa ya kuwa kwenye makao makuu, lakini kwa sifa ya zaida ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokea mkoa wa Kagera  na kigezo kingine chochote kilichoufanya uwanja huo kuchaguliwa kwa michuano hiyo ni dhahiri kwamba hakukupaswa kuwa na upungufu huo ulioonekana na kututia doa  duniani kote.

Ukiangalia kwenye mitandao ya kimataifa utaona aibu hiyo ya mgonjwa kupandishwa kwenye gari za Zimamoto, kama ilikosekana gari hiyo ninawasiwasi pia hata wale wahudumu wa huduma ya kwanza hawakuwa wa kiwango  kinachostahili kuwepo uwanjani hapo.

Mara zote watu wa huduma ya kwanza kwenye viwanja vyetu wao hujulikana kwa kazi ya kumbeba mchezaji kwenye machela na kumtoa nje ya uwanja, huduma zote huenekana zikifanywa na madaktari wa timu husika, isipokuwa Uwanja wa Taifa ambapo pengine ndiyo huwa wapo madaktari maalum wanaoshughulika na huduma ya kwanza mbali na wale wadada na wakaka  wanaiongiaga na machela pale uwanjani.

Kuna kila sababu ya TFF kulifanyia kazi suala hili la huduma ya kwanza hasa kwenye michuano mikubwa kama hii, lakini pia kutia msisitizo zaidi wa uwezo wa huduma ya kwanza ya kueleweka kwenye michuano mbalimbali inayosimamiwa na vyama vya wilaya na mikoa.

Leo hii tumempoteza Ismail, mapenzi ya Mungu yametimia, lakini nani anajua? Pengine tungeweza kukoa maisha yake kama kweli kungekuwepo na huduma ya kwanza ya uhakika pale uwanjani. Mungu atunusu na majanga na aina hii. Mungu ailaze roho ya marehemu Ismail mahali pema Peponi. Amen.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -