Tuesday, November 24, 2020

CAF wakanusha taarifa za kifo cha Song

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

CAIRO, Misri

SHIRIKISHO la Soka la Afrika (CAF), wamechukizwa na wamekanusha taarifa za kifo cha mchezaji wa zamani wa Cameroon, Rigobert Song.

Kumekuwa na uvumi kwa siku kadhaa sasa kwamba Song amefariki tangu Ijumaa, Oktoba 7 mwaka huu baada ya kupata kiharusi siku mbili kabla ya uzushi huo wa kifo chake.

Lakini mwandishi wa michezo wa Afrika, Gary Al-Smith, ambaye anafanya kazi BBC na CNN, alisema mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba Song hajafanya na ameanza kuzungumza.

“Vyombo kadhaa vya habari viliripoti kwamba Rigobert Song hajafa. Alipunga mkono asubuhi ya leo (Jumamosi) na aliweza kuzungumza,” alisema Al-Smith.

“Rais wa CAF, Issa Hayatou, atamtembelea Rigobert Song katika hospitali ya La Pitie Salpetriere mjini Paris, Ufaransa (Jumamosi). Song ana tatizo kwenye ubongo si kiharusi,” aliongeza Al-Smith, alipokuwa akizungumza juzi.

Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool na West Ham, aliugua ghafla wiki iliyopita na kulazwa kwenye chumba cha uangalizi maalumu nchini kwao Cameroon.

Alipelekwa kwenye Hospitali ya Yaounde Central nchini Cameroon, baada ya hali kuwa mbaya na kukaa kwenye chumba hicho cha uangalizi maalumu kwa siku mbili kabla ya kusafirishwa mpaka Ufaransa kwa matibabu zaidi.

Song alionekana akiwapungua mashabiki wakati anaondoka uwanja wa ndege wa Yaounde akielekea Ufaransa. Mkurugenzi wa kituo cha dharura, Dk. Louis Joss Bitang A Mafok, alisema kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40 amepata ugonjwa wa kutokwa damu kwenye ubongo.

Naye Waziri wa Afya wa Cameroon, Andre Mama Fouda, amethibitisha kwa vyombo vya habari akisema: “Song amepelekwa kwenye Hospitali ya Pitie Salpetriere mjini Paris, ambapo ataendelea kufanyiwa matibabu. Pia tunashukuru kwa rais kuagiza kwamba, Song afanyiwe vipimo maalumu mpaka arejee kwenye hali yake ya kawaida.”

“Tunawapongeza madaktari wa Cameroon na tunamwombea Rigobert Song na atapona mapema.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -