Friday, December 4, 2020

CAMEROON WALIVYOPITA NJIA NGUMU KUTIMIZA NDOTO YA MIAKA 15

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

LIBREVILLE, Gabon

MICHUANO ya fainali za Mataifa Afrika ilimalizika juzi usiku ambapo Cameroon walifanikiwa kunyakua taji hilo mbele ya Misri.

Katika mtanange huo wa fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Stade d’Angondje, Cameroon walipata ushindi wa mabao 2-1.

Mafarao wa Misri walikuwa wa kwanza kuziona nyavu za Cameroon katika dakika ya 22 kupitia kwa kiungo wao Mohamed Elneny.

Bao hilo lilisawazishwa na Nicolas Nkoulou kabla ya Vincent Aboubakar aliyetokea benchi kuipa ushindi Misri kwa bao lake la dakika za majeruhi.

Kwa ubingwa huo, Cameroon linakuwa taifa la pili kwa kuchukua mara nyingi taji la mashindano hayo.

Taji lao hilo la tano linawafanya kuwa nyuma ya Misri ambao wamelinyakua mara saba.

Hii ni mara ya kwanza kwa Cameroon kuwafunga Misri katika mchezo wa fainali licha ya kukutana nao mara tatu.

Pia, ikumbukwe kuwa mara yao ya mwisho kuingia fainali ya Afcon ilikuwa mwaka 2008 na kipindi hicho Cameroon ilikuwa ikiongozwa na staa Samuel Eto’o.

Cameroon walipoteza mchezo huo mbele ya Misri ambapo walikubali kichapo cha bao 1-0 katika mchezo huo uliochezwa jijini Accra, Ghana.

Mchezo wa juzi ulichezwa huko Libreville, mji unaotajwa kuwa na Wacameroon wengi pale Gabon. Kwa kunyakua taji hilo, Cameroon wamejishindia kitita cha dola za Marekani, milioni nne huku wenzao Misri wakilamba dola milioni tatu.

“Nimefurahi kuchukua ubingwa wa Afcon na wachezaji wamenikuna. Hawa si wachezaji wangu, ni marafiki zangu,” alisema Mbelgiji Hugo Broos anayeinoa Cameroon.

Hata hivyo, haikuwa safari ndogo kwa Cameroon kuchukua taji hilo kwani imewachukua miaka 15 kulipata.

Itakumbukwa kuwa katika fainali za mwaka 2012 na 2013, Cameroon walishindwa kufuzu na hata walipoingia kwenye zile za mwaka 2015 waliishia hatua ya makundi.

“Ni mtu wa muujiza. Timu imezaliwa upya,” alisema beki wa kikosi hicho, Michael Ngadeu, alipokuwa akimzungumzia kocha Broos.

“Wengi hawakuwa na imani naye, nakiri hilo. Wacameroon wengi walimkosoa. Lakini leo nadhani amekuwa shujaa. Anapaswa kupewa medali kwa alichokifanya.

Nyota ya mafanikio katika fainali za mwaka huu ilianza kuonekana katika mechi za kuwania kufuzu ambapo walishinda michezo yote ya hatua ya makundi.

Hata hivyo, walipokata tiketi, Cameroon walijikuta wakikumbwa na mkosi wa baadhi ya mastaa wake wanaokipiga barani Ulaya kukataa kujiunga na timu hiyo.

Nyota hao ni pamoja na Joel Matip, Allan Nyom na Eric Maxim Choupo-Moting.

Lakini, baada ya kukosekana kwa mastaa hao, timu hiyo ilianza kwa mwendo wa kusuasua kwenye fainali hizo za Gabon.

Katika mchezo wao wa kwanza, waliambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Burkina Faso.

Cameroon walianza kupata bao katika dakika ya 35 kupitia kwa Benjamin Moukandjo kabla ya Issoufou Dayo kuisawazishia Burkina Faso.

Mchezo uliofuata wa Kundi A, Cameroon waliendelea kutota baada ya kutofungana na wenyeji Gabon.

Cameroon walianza kupata ushindi katika mchezo wao wa tatu ambapo waliichapa Equatorial Guinea mabao 2-1.

Matokeo hayo yaliwawezesha kutinga robo fainali ambapo walipata ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Senegal na kisha kuwachapa Ghana mabao 2-0 katika mchezo wa nusu fainali.

Cameroon walikuwa wakimtegemea mlinda mlango wao Benjamin Moukandjo na kinda Christian Bassogog, ambaye ametajwa kuwa mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa fainali za Afcon 2017.

 ‘Fist Eleven’ ya Afcon 2017

Mlinda mlango: Fabrice Ondoa (S. Atletico, Cameroon)

Mabeki: Odou Kara Mbodji (Anderlecht, Senegal), Ahmed Hegazy (Al Ahly, Misri), na Michael Ngadeu (Slavia Prague, Cameroon).

Viungo: Charles Kabore (FC Krasnodar, Burkina Faso), Daniel Amartey (Leicester City, Ghana), Bertrand Traore (Ajax, Burkina Faso), Christian Atsu (Newcastle, Ghana), na Mohamed Salah (Roma, Misri)

Washambuliaji: Christian Bassogog (AaB, Cameroon), na Junior Kabananga (Astana,  DR Congo)

Kocha : Hugo Broos (Ubelgiji, Cameroon)

Zawadi za Afcon 2017

  1. Cameroon (dola mil 4)
  2. Misri (dola mil 3)
  3. Burkina Faso (dola mil 2)
  4. Zilizoishia robo (dola 700,000)
  5. Zilizoishia 16 bora (dola 500,000)

Tuzo zilizotoka

  1. Mchezaji Bora wa michuano- Christian Bassogog (Cameroon).
  2. Nyota wa mchezo wa fainali: Benjamin Moukandjo (Cameroon).
  3. Tuzo ya timu yenye nidhamu: Misri.
  4. Mfungaji Bora Afcon: Junior Kabananga (DRC).
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -