Friday, December 4, 2020

CHANGAMOTO HIZI ZIFANYIWE KAZI MZUNGUKO WA PILI VPL

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA OSCAR ASSENGA, TANGA


WAKATI mzunguko wa pili wa Ligi kuu  Tanzania Bara ukitarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 17, mwaka huu kwenye viwanja mbalimbali nchini baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza, yapo mambo yaliyojitokeza yanayopaswa kufanyiwa kazi na Shirikisho la Soka nchini (TFF) ili kuipa heshima ligi hii.

Hadi mzunguko wa kwanza unapomalizika, kila timu imevuna kile ambacho ilikipanda kutokana na maandalizi waliyoyafanya kwenye awamu ya kwanza ya maandalizi ya michuano hiyo.

Matokeo ya mchezo wa soka hayawezi kupatikana hivi hivi, yanatokana na maandalzi yaliyofanyika kuanzia katika ngazi ya usajili, mazoezi na mambo mengine muhimu kwa timu kupata ushindi. Kwa Tanzania hata kama timu imesajili wachezaji wa kimataifa lakini kama ina maandalizi duni, haiwezi kufanya maajabu kwani viwango vya wachezaji wetu vinafanana kwa kiasi kikubwa.

Pamoja na mambo mengine, lakini katika mzunguko wa kwanza zipo changamoto kadhaa ambazo zimejitokeza na kuibua malalamiko, jambo ambalo wakati mwengine limesababisha wadau hasa mashabiki kukasirika na kuanza kuisusa ligi  hiyo kwa kutoingia viwanjani.

Suala la kwanza ambalo limekuwa kero kubwa si kwa klabu pekee hata kwa mashabiki, ni jambo la pangua pangau ya ratiba ya michuano ya ligi kuu; hili nalo si kwamba halifahamiki bali wakati mwengine limekuwa likifanya mashindano hayo kupoteza ladha na kuonekana kama vile bonanza.

Ratiba ya mashindano ya kimataifa inayotambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), inaonyesha wazi yatafanyika lini, lakini bado kwa Tanzania utakuta mechi hizo zinasababisha kuharibu ratiba za mechi zetu za ligi kuu na zaidi kuna timu chache tu zinapanguliwa ratiba zao na  nyingine zinaendelea na ligi.

Licha ya hilo, lakini jingine kubwa ni kutokuwa na umbali baina ya mechi na mechi ambazo timu zetu zimekuwa zikicheza, jambo ambalo linaondoa msisimko na ushindi kwenye baadhi ya michezo, kwani timu zinapocheza Jumapili na Jumatano na kutakiwa kucheza tena, inaondoa ari na ushindani.

Tujiulize timu inapangwa kucheza Jumapili Mbeya, timu hii inawezaje kufika Bukoba mapema na ikawahi kucheza mechi Jumatano? Mpangilio wa ratiba si mzuri  kabisa na hii inasababisha ama mechi kuahirishwa au timu kulazimika kucheza ikiwa na uchovu mkubwa.

Waamuzi
Hapo ndipo ambapo unaweza kusema kuna shida kubwa sana, hali inayosababisha wapenzi na wadau wa soka hapa nchini kulichukia soka letu, kwani wapo baadhi ya waamuzi ambao wanakwenda viwanjani wakiwa na matokeo mkononi, jambo ambalo linawafanya kushindwa kuzitendea haki sheria 17 za mchezo huo.

Mashabiki wa soka wamekosa imani na waamuzi wetu kutokana na kuboronga kwao kwa kiasi kikubwa, jambo ambalo katika baadhi ya mechi imeshuhudia mashabiki wakichukua sheria mkononi kuwaadhibu waamuzi au kuharibu miundombinu ya viwanja na kurusha mawe viwanjani.

Ni vyema Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likafanya kazi ya ziada kuhakikisha waamuzi wanachezesha soka kwa kuzingatia sheria 17, lakini pia kwa haki ili hatimaye bingwa wa ligi apatikane kwa haki.


Vyombo vya Ulinzi na Usalama

Kama umekuwa mshabiki wa muda mrefu unahudhuria viwanjani, utaungana nami kuwa wapo baadhi ya askari wanakwenda viwanjani si kwa ajili ya kulinda usalama, bali kutimiza matakwa ya ushabiki wa timu zao wanazozipenda.

Kumekuwa na matukio mengi yanatokea kwenye viwanja vya soka hapa nchini licha ya uwepo wa askari hao, lakini kunatokea uharibifu mkubwa wa mali na hata wakati mwengine kusababisha majeraha kwa baadhi ya mashabiki wanaokuwa wakijitokeza kushuhudia michezo.

Ulanguzi wa Tiketi

Ulanguzi wa tiketi kwa wapenzi na mashabiki wa soka hapa nchini  hasa kwa viwanja vya mikoani ambako mfumo wa Kielektroniki haitumiwi, umekuwa ukishamiri na umekuwa kilio cha kila siku kwa mashabiki wa soka.

Kutokana na uwepo wa wingi wa mashabiki hasa kwenye mechi zinazohusisha timu kongwe za Yanga na Simba zenye mashabiki wengi, mara nyingi kumeripotiwa vurugu zinazosababishwa na kile kinachoelezwa kwamba tikezi zimekwisha au kupanda bei kwa tiketi muda mchache kabla ya mchezo kuanza.

TFF inapaswa kujenga msingi imara katika kudhibiti hili, kwani limekuwa janga kubwa katika awamu ya kwanza na misimu iliyopita, hivyo basi ni vyema kama hili litadhibitiwa ili mashabiki waweze kupata fursa ya kuangalia mechi kwa gharama halisi zilizopangwa.

Viporo
Jambo hili limekuwa ni wimbo uliodumu kwa kipindi kirefu kwenye michuano ya ligi kuu na Ligi Daraja la kwanza bila kupatiwa ufumbuzi, kitendo ambacho wakati mwengine kinasababisha kupoteza ladha ya mashindano husika lakini pia kuondoa ushindani.

TFF ijitahidi kuepusha viporo hasa katika raundi hii ya pili, timu zote zicheze mechi kwa wakati ili kuepusha dhana ya kupanga matokeo kwani tunafahamu soka letu kwa timu kuwa kiporo ni fursa adhimu ya kuifanya timu ifanye inachokitaka. Ile inayohitaji ubingwa inajipanga hata nje ya uwanja na ile nyingine inakuwa tayari kupokea chochote hasa kama haiathiriki kwa namna yoyote na matokeo ya mechi hiyo.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -