Monday, January 18, 2021

CHANGAMOTO HIZI ZITATULIWE MCHEZO WA TENISI

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

MCHEZO wa tenisi ni moja kati ya michezo inayokuwa kwa kasi sana duniani kote. Hadi sasa mataifa zaidi ya 211 yanacheza mchezo huo katika ngazi ya mashindano na yanatambulika na shirikisho la kimataifa la mchezo huo (ITF).

Wingi wa mataifa yanayocheza mchezo huo yanaufanya kuwa moja kati ya michezo mikubwa zaidi duniani, ukiwa ni mchezo wenye wapenzi wengi sana sehemu mbalimbali huku Tanzania ikiwa ni moja ya nchi zinazoucheza na kuwa mwanachama wa ITF.

Kwa Tanzania mchezo huo unakuwa lakini kwa kiasi kikubwa umekumbwa na changamoto mbalimbali za kiuongozi ambazo zimejitokeza katika awamu hii ya uongozi wa chama hicho, jambo ambalo linahatarisha maendeleo mazuri  yaliyokuwa yakipatikana.

Hadi sasa Chama cha Mchezo wa Tenisi Tanzania (TTA), ni kama hakina uongozi kwani viongozi wa juu wamejiuzulu na chama kimebakiwa na katibu mkuu na msaidizi wake na wajumbe wawili pekee. Jambo ambalo limesababisha shughuli za chama kuzorota ikiwamo kukosekana kwa mashindano na pia kuathiri ushiriki wa Tanzania katika michuano ya kimataifa ya tenisi.

BINGWA tunafahamu kwamba kama hakuna uongozi thabiti si rahisi japo kupiga hatua, hivyo basi mchezo wa tenisi kwa sasa umekwama kutokana na ukweli kwamba kumekuwa na changamoto kubwa ya kiuongozi kwenye chama hicho.

Tungependa kuona Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT), kushughulikia suala hili kwa haraka ili kuhakikisha chama hicho kinapata viongozi na kuanza mchakato wa kuurejesha mchezo huo kwenye chati yake, kwani licha ya kuwapo kwa wachezaji wengi wazuri katika timu za kawaida na ile ya walemavu Tanzania, inaonekana kupoteza hadhi na nafasi yake iliyokuwa imejijengea kwenye mchezo huo kutokana na kukosekana kwa mwongozo.

Kwa sasa mchezo wa tenisi unapendwa sana na kwa Tanzania ulishaanza kupiga hatua kwa namna mbalimbali, vijana wengi wanacheza na wengine wangependa kuingia kujifunza mchezo huo, lakini changamoto zilizopo hivi sasa zinakatisha tamaa kwa wachezaji waliopo na wale chipukizi wanaojifunza mchezo huo, kwani hakuna mashindano yoyote ya maana ya ndani zaidi ya mazoezi tu.

BINGWA tukiwa kama wadau namba moja wa michezo nchini Tanzania, tungependa kuona changamoto hizi kwenye mchezo wa tenisi zinatatuliwa haraka, TTA inapata viongozi wapya mapema ili kuendeleza gurudumu la mchezo huo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -