Friday, December 4, 2020

CHANZO CHA WENGER KUMUWEKA BENCHI SANCHEZ CHABAINIKA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

LONDON, England

KWA lugha nyingine unaweza kusema  kwamba  siri imefichuka, baada ya  taarifa kuvuja kuhusu uamuzi wa kocha wa Arsenal,  Arsene Wenger, kuamua kumuweka benchi straika wake, Alexis Sanchez, wakati wa mechi yao dhidi ya Liverpool iliyopigwa Jumamosi iliyopita.

Vyombo vya habari nchini Uingereza vilinasa nyeti hizo jana zikieleza kuwa chanzo cha kocha huyo kutompanga Sanchez kipindi cha kwanza ni baada ya kukwaruzana na kocha huyo pamoja na wachezaji wenzake wakiwa mazoezini wakijiandaa na mtanange huo.

Kwa mujibu wa gazeti la  Daily Telegraph, Sanchez aliondoka kwa hasira mazoezini, baada ya kukwaruzana na wachezaji wenzake ikiwa ni siku moja kabla ya mechi hiyo.

Gazeti hilo liliripoti kuwa, mkwaruzani huo unaweza kumfanya raia huyo wa Chile kuitema Arsenal mwishoni mwa msimu huu na huku timu za  Paris Saint-Germain  na  Juventus zikitajwa kuwinda saini yake.

Msimu huu Sanchez ameshafunga mabao  17 katika mechi  26  za ligi, lakini siku hiyo akajikuta akiwekwa benchi wakati wa mchezo huo uliopigwa katika dimba la  Anfield, ambapo ilishuhudiwa  Liverpool wakiwa mbele kwa mabao mawili.

Kipindi cha pili Wenger alimuingiza  Sanchez, ambapo aliweza kutoa mchango ambao uliosababisha kupatikana  bao lililofungwa na  Danny Welbeck.

Kutokana na uamuzi huo wa Wenger, wachambuzi wengi wa soka walimkosoa sana, lakini kwa mujibu wa Telegraph, wachezaji wengi wa Arsenal wanamuunga mkono kocha huyo mwenye umri wa miaka  67 kwa kumtosa  Sanchez katika kikosi hicho cha kwanza.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -